Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Clement Berege pamoja na Balozi wa Japan
Masaki Okada wakiweka sahihi ya msaada wa fedha kwa ajili ya mradi wa uwekwaji
mashine ya kukamulia mafuta ya Alizeti, Chato. Huku Waziri wa Ujenzi ambaye pia
ni Mbunge wa Chato Mhe. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo
balozi Okada amesema serikali ya japan imeamua kutoa msaada wa dola za Marekani
95,124 sawa na shilingi milioni 165 za Tanzania kugharamia mradi huo.
“Mradi huu ni wa kipekee
katika miradi toka mfoko wa grant assistance for grassroots human security
projects GGHSP kwani unalenga kuhamasisha kilimo cha alizeti wilayani chato na
hivyo kuibua fursa mpya za ajira na
kuwawezesha wananchi kutumia mafuta yasio na lehemu” ,amesisitiza balozi Okada.
Akizungumza katika hafla hiyo
mbunge wa chato, ambae pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli
amemshukuru balozi Okada kwa misaada mbalimbali anayoitoa hapa nchini na katika
jimbo la chato ili kuibua fursa za kiuchumi na kuharakisha maendeleo.
Amewataka wajenzi wa kiwanda
hicho kukijenga kwa viwango vya ubora unakubalika na kumaliza kazi hiyo kwa
wakati ili kuanza uzalishaji wa mafuta kwa haraka .
“kiwanda hiki kitakapokamilika
kitakuwa na uwezo wa kutengeneza lita 1600 za alizeti kwa saa moja na kukamua
gunia 80 za alizeti na hivyo kuwezesha mafuta ya alizeti kusambazwa ndani na
nje ya nchi na kukuza uchumi”, amefafanua waziri Dkt. Magufuli.
Naye mkurugenzi wa halamashauri
ya wilaya ya chato Clement Berege
amemhakikishia balozi kuwa msaada wa
kiwanda cha kutengeneza mafuta ya alizeti utasimamiwa kikamilifu ili uwe na
manufaa kwa jamii ya chato na wananchi kwa ujumla.
Katika hatua nyingine balozi
Okada amesaini mkataba wa kutoa magari mawili ya kusafirisha wagonjwa ambulance
katika hospitali ya taifa ya muhimbili ili kupunguza changamoto ya usafirishaji
wagonjwa.
Naye kaimu mkurugenzi mtendaji
wa hospitali ya taifa ya muhimbili Dkt. Hussein kidanto amemshukuru balozii wa
japan kwa msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 70 na kuahidi hospitali
hiyo iko kwenye mkakati wa kuanzisha kitengo cha ambulance ili kusafirisha kwa
haraka wajawazito, wagonjwa na waathirika wa ajali na hivyo kuwafikisha katika
hospitali hiyo kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment