Mkulima toka mkoani Pwani Ramadhani Dilunga
miaka 53 na Mwalimu mstaafu wa Mtwara bw, Namtapika Kilumba (60) ni miongoni
mwa Watanzania watatu walioibuka washindi kwenye droo ya kwanza ya Airtel Yatosha
Zaidi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Washindi hao kila mmoja ameibuka mshindi wa gari aina ya IST Toyota mpya, ikiwa ni siku chache tu tangu kuzindulia kwa promosheni hiyo.
Airtel Tanzania wiki iliyopita ilitangaza dhamira yake ya kuwazawadia wateja wake wanaojiunga na bando za Airtel Yatosha gari moja kila siku kwa siku 60 ambapo mwishoni mwa wiki tayari magari matatu yalipata washindi.
Washindi hao kila mmoja ameibuka mshindi wa gari aina ya IST Toyota mpya, ikiwa ni siku chache tu tangu kuzindulia kwa promosheni hiyo.
Airtel Tanzania wiki iliyopita ilitangaza dhamira yake ya kuwazawadia wateja wake wanaojiunga na bando za Airtel Yatosha gari moja kila siku kwa siku 60 ambapo mwishoni mwa wiki tayari magari matatu yalipata washindi.
Balozi wa Airtel, na msanii maarufu wa filamu
nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ndiye aliyekuwa na jukumu la kuwapigia simu
washindi na kuwapa taarifa hizo nzuri kwa mwaka 2015 chini ya Mkaguzi
Mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid
Wa kwanza kupigiwa alikuwa Namtapika Kilumba wa
Mtwara mwenye umri wa miaka 60 na aliposikia sauti ya Lulu ikisema; “Ninapenda
kukutaarifu kuwa umeshinda gari aina ya IST Toyota mpya baada ya kujiunga na
Airtel Yatosha Zaidi”, alipiga kelele kwa furaha na mara moja akamshukuru Mungu
pamoja na Lulu.
“Mungu wangu. Sikutarajia kabisa kama leo
ningepata taarifa nzuri kama hizo! Kumbe ni kweli kuwa mtu yeyote anaweza
kushinda promosheni ya Airtel? siamini,” alisema … kwa njia ya simu; na hata
wengine pia waliopigiwa simu na Lulu walikuwa na maoni yanayoshabihiana na
hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya droo
hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, alisema: “Haya ndio kwanza
magari matatu tu. Bado mengine 57 yote aina ya IST Toyota mapya kabisa yapo
‘showroom’. Ndani ya 60 za mwaka huu, wateja 60 wa Airtel watakuwa wakiishi
maisha mapya katika dunia ya ndoto zao.
“Watakuwa ni wamiliki wa magari kwa kujiunga na
bado za Airtel Yatosha zaidi kwa kupiga simu *149*99# na kujiunga. Hebu
fikiria, unapata muda wa maongezi zaidi, vifurushi vya internet zaidi, SMS
zaidi na bado unakuwa na nafasi ya kujishindia gari.”
Mmbando alimtaja mshindi mwingine kuwa ni
Mwajabu Churian mwenye umri wa miaka 27 na mfanyabiashara anaeishi Mbagala huku
akiwasihi wateja wa Airtel kuendelea kufurahia huduma hiyo.
0 comments:
Post a Comment