Meneja Usambazaji na Matawi, Bi. Masala Korosso
wa FNB Tanzania akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa matawi
mapya ya benki hiyo yaliyofunguliwa Sinza Kijiweni na Mbagala Zakhem kwa lengo
kusogeza huduma kwa wateja pamoja na kuhudumia biashara ndogo na za kati
zinazokua kwa kasi katika maeneo hayo. Kushoto ni Meneja Huduma za Rejareja wa
Benki hiyo Emmanuel Mongella
Meneja Huduma za Rejareja wa FNB Tanzania Emmanuel
Mongella Meneja Usambazaji akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi
wa matawi mapya ya benki hiyo yaliyofunguliwa Sinza Kijiweni na Mbagala Zakhem
kwa lengo kusogeza huduma kwa wateja pamoja na kuhudumia biashara ndogo na za
kati zinazokua kwa kasi katika maeneo hayo. Kushoto ni Meneja Matawi, Bi. Masala
Korosso.
**************
First National
Bank imeongeza huduma zake kwa maeneo mengi zaidi ya jiji la Dar es salaam kwa
kufungua matawi mawili mapya katika maeneo ya Sinza na Mbagala. Hii inaifanya
benki hiyo kuwa na jumla ya matawi saba yaliyofunguliwa katika kipindi cha
miaka mitatu.
Meneja wa
Huduma za Rejareja wa First National Bank, Emmanuel Mongella amesema kuwa
matawi mapya yatakidhi mahitaji ya huduma za kibenki kutoka benki hiyo ambayo
yanaendelea kuongezeka na matawi haya yatahudumia wateja wa reja reja na wateja
wa biashara katika maeneo haya ambayo yana biashara ndogo na za kati zinazokua
kwa kasi sana. Matawi haya yanakuja na huduma
zilizolenga kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja na jumuiya za biashara
katika maeneo hayo.
"Tuna
imani kuwa matawi haya yatafanikiwa na tuna mipango kabambe ya kufungua matawi
kwenye maeneo mengine tukianza na Arusha na Mwanza kabla ya mwisho wa mwaka
huu,” alisema Mongella.
Meneja
Usambazaji na Matawi, Masala Korosso alisistiza kwamba benki imechagua kuwekeza
katika maeneo haya kutokana na ukuaji kasi wa jiji la Dar es salaam na kuongeza
kuwa tawi la Sinza liko eneo la Kijiweni
na tawi la Mbagala liko eneo la Rangi Tatu.
Alisema kuwa
Sinza na Mbagala ni maeneo muhimu kuwekeza na ndio maana FNB imeona ni wakati
muafaka kuanzisha huduma zake kwenye maeneo hayo. “Kwa pamoja Sinza na Mbagala ni
maeneo ambayo yanakua sana kiuchumi na hii imetulazimu kuhakikisha uwepo wa FNB
katika maeneo haya”.
Ufunguzi wa
matawi haya utaongeza huduma ambayo tayari inatolewa na FNB kupiti tawi la Kariakoo
lililoko mtaa wa Uhuru, tawi la Makao Makuu eneo la Posta, tawi la Viwandani
lililopo Quality Centre, Peninsula lililopo Oysterbay na Kimweri lililopo
Msasani.
0 comments:
Post a Comment