Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri,Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Manaibu Waziri wapya aliyowaapisha Ikulu Dar es Salaam jana. Pia katika picha yupo waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi, balozi Ombeni Sefue.
*********
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo
ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo
Ameliapisha jioni hii Ikulu,Jijini Dar es Salaam.
Akitangaza
uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu
Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza
nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa
Sospeter Muhongo.
Profesa
Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti
ya Tegeta Escrow.
Kwa
upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema leo, kwa kile
alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya
kuendelea na malumbano ya Escrow.
Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.
Akitangaza Mabadiliko hayo,Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.
MAWAZIRI
1. Mh. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini
2. Mh. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu)
3.Mh. Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
4. Mh. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.Mh. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
6.Mh. Steven Wasira - Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
8.Mh. Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge
MANAIBU WAZIRI
1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Mazingira
2. Mh. Angela Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
3. Mh. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4. Mh. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5 . Mh. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini
0 comments:
Post a Comment