Nafasi Ya Matangazo

January 21, 2015

 Kamishana wa Polisi Oparesheni na Mafunzo, Paulo Chagonja, katika picha hii ya maktaba akizungumzia tukio la uvamizi wa kituo cha Polisi Ushirombo.
*****
Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi yamevamia kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua Askari wawili na kupora silaha (bunduki) zilizokuwepo kituoni hapo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo,huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar  aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.

Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika Tukio la uvamizi, kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani

Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, Shotgun  1, silaha 2 za mabom ya machozi na risasi 60 za smg.
Hili ni tukio la tatu  katika kipindi cha miezi saba kwa majambazi kuvamia kituo cha polisi. Juni 11 204, mwaka huu askari polisi mmoja aliuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia Kituo Kidogo cha Polisi cha Kimanzichana mkoani Pwani kisha kupora bunduki tatu aina ya SMG na risasi zake.
Usiku wa Septemba 6, 2014 Askari wa wawili wa Jeshi la Polisi kituo Kikuu cha Ushirombo kilichopo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita walifariki huku wengine wawili wakijeruhiwa baada ya kundi la majambazi kuvamia kituo hicho na  Aidha katika tukio hilo, majambazi hayo yalifanikiwa kuchukua baadhi ya silaha zilizopo kituoni hapo.
Posted by MROKI On Wednesday, January 21, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo