Na Michael
Machellah.
MPAMBANO wa ngumi za kirafiki kati ya Thomasi Mashali
kutoka Manzese jijini Dar es Salaam na Abdalah Pazi kutoka Mwananyamala
limetoka sare (Technical draw-dt) baada ya Thomas Mashali kuvuja damu nyingi
toka juu ya jicho la kushoto alilopasuliwa kwa konde zito na mpinzani wake
Abdala Pazi(Dullah Mbabe) mwishoni mwa raundi ya pili.
Raundi ya
tatu mwanzoni Mashali alishambuliwa zaidi kiasi cha kukosa muelekeo ambapo pia
damu zilizidi kutoka kushoto kwa jicho lake ndipo mwamuzi wa mpambano, Hakwe
Mtulya alisimamisha mpambano kwa matibabu na baada ya Daktari kufanya uchunguzi
wa kina ikadhihirika Mashali hawezi kuendelea na pambano hilo kwani damu
zilikuwa zinatoka zaidi eneo la jeraha.
Kwa hatua
hiyo mpambano ulikuwa ni droo kwa mujibu wa sharia za ngumi (Proffesional
Boxing) kuwa mpambano unaoshia chini ya roundi ya nne ukiwa haujakamilika kwa
ajali hiyo ni droo(Technical draw-dt).
Kabla ya
matokeo hayo kutangazwa mashabiki wa ngome ya mashali walianzisha fujo
iliyopelekea kuharibu viti,meza na watu kuumizwa ovyo ililazimika matokeo
ktotangazwa na Katibu Mkuu wa Ngumi za kulipwa Tanzania(Tanzania Proffessional
Boxing), Ibrahim Kamwe(Big Right) aliyathibitisha haya yote.
Mpambano
wa
Thomasi Mashali na Abdalah Pazi ulikuwa ni wa kirafiki wa round
inane(8), kutafuta kadi unaowawezesha kugombania Ubingwa ulifanyika
juzi tarehe 1,1,2015
katika Ukumbi wa Manzese France Corner jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment