Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Pujini wilayani Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Katika mkutano huo, Kinana alitumia staili yake ya kuwakataza wananchi kumshangilia akiwataka wamsikilize vizuri maneno aliyokuwa akizungumza kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ambapo alimsifia Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kwa uchapakazi wake kwa kuwaletea maendeleo wananchi katika visiwa vya Pemba na Unguja.
Alisema wakati wa uongozi wake amejenga barabara nyingi za lami, miradi ya maji, Afya na elimu karibu kila kona ya visiwa vya Pemba na Unguja, lakini wakati anafanya mambo yote hayo wapinzani wakiwemo viongozi wa CUF na wafuasi wao wanajifanya hawayaoni maendeleo hayo.
Alisema Serikali YA ccm iliyo chini ya Rais Dk. Shein imepeleka umeme, miradi ya maji na barabara za lami hata katika Jimbo la Mtambwe alikozaliwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.
Kinana amelaani kitendo cha CUF kuwaita makafiri watu wotinginee wanaokihama hicho kwenda CCM na vyama vingine, ambapo ameomba viongozi wa dini kulikemea jambo hilo, akidai hakuna binadamu mwenye haki ya kumwita mwenzie kafiri isipokuwa Mungu.
Pia alikemea vikali tabia isiyo sahihi iliyozuka ya kuwatenga waliokuwa wana CUF na kuamua kujiunga na CCM na vyama vingine, akidai kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote akipendacho.
Wananchi wakishangilia wakati Kinana akiingia kuhutubia katika mkutano huo.
Msafara wa Komredi Kinana ukikagua shamba la miti la Ushirika wa Hatugombani Kata ya Kilindi wilayani Chakechake. Katika shamba hilo ambalo Kinana alishiriki kupanda miti lilianzishwa kwa msaada wa TASAF. Zaidi ya miti 34,000 imependwa.
Aliyekuwa Mwanachama wa CUF na kuhamia CCM, Gharib Bedui Hamisi akionesha kadi yake kabla ya kumkabidhi Komredi Kinana aliyemkabidhi kadi ya CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Pujini, Chakechake, Pemba. Hamis alielezea katika mkutano huo kuwa baada ya kutangaza kuhamia CCM AMATENGWA NA FAMILIA YAKE PAMOJA NA BAADHI YA MARAFIKI ZAKE.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mwanajuma Majid Abdallah akishiriki kupanda miti katika shamba la Ushirika wa Hatugombani.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Daud Ismail akishiriki kupanda mti katika shamba la Ushirika wa Hatugombani.
.Mwanachama mwingine wa CU aliyehamia CCM, Said Abdalah Ibrahim akionesha kadi ya CUF kabla ya kumkabidhi Komredi Kinana ili apatiwe kadi ya CCM
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Mchangani Jimbo la Wawi.Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.
Wafuasi wa CCM wakimlaki Kinana huku wakiwa na picha za Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
Komredi Kinana akishirikiana na Mwenyekitri wa Chama cha ADC Chakechake, Mohamed Said Abdalah (kulia) na Mwenyekiti wa Chadema Uwandani Kombo Ali Abdalah aliposhiriki ujenzi wa Ukumbi wa shule ya Sekondari ya Uwandani katika Jimbo la Wawi, Chakechake.
Kinana na viongozi wengine wa chama na serikali wakiondoka baada ya kushiriki kupanda miti katika shamba la Ushirika la Hatugombani.
Kinana akishiriki kuotesha miche ya mikarafuu katika shamba la Kikundi cha Hatukosani Jimbo la Chakechake
Sehemu ya miche ya karafuu ikiwa imeoteshwa katika bustani ya Kikundi cha Hatukosani katika Kata ya Chanjanjawili, Chakechake
Sehemu ya Mji wa Chakechake, Makao Makuu ya Mkoa wa Kusini Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Pujini/
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Pujini, Wilaya ya Chakechake, Pemba
Kinana akipanda mti akatika shamba la miti la Ushirika wa Hatugombani, Shaia ya Kilindi, Chakechake, Pemba.
0 comments:
Post a Comment