Nafasi Ya Matangazo

January 22, 2015

Na Faustine Ruta, Mwanza
Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) Imewasili leo Jijini Mwanza, Januari 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba hapa Mjini Mwanza.
Amavubi imetua na msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi na kufikia kwenye kwenye hoteli ya JB Belmont.
Wachezaji baadhi wa Timu ya Amavubi ya Nchini Rwanda walipa picha ya pamoja kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza jioni ya leo, Tayari kwa Mtanange wa kirafiki wa Kitaifa kesho na Timu ya Hapa Nchini ya Taifa Stars Maboresho.(Katikati) ni Haruna Niyonzima akitokelezea kwenye Picha pamoja.

 
Haruna Niyonzima
 

Haruna Niyonzima akiwa na VIongozi wa Timu hiyo Amavubi

Wachezaji wa Timu ya Amavubi ya Nchini Rwanza wakiwa wamekaa kwenye Uwanja CCM Kirumba huku wakiunda mbinu ya kuifunga Timu ya Taifa Stars Maboresho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Mwandishi wa bukobasports.com nae alipata picha ya pamoja na Wachezaji wa Rwanda (AMAVUBI) leo hii jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Posted by MROKI On Thursday, January 22, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo