Nafasi Ya Matangazo

December 08, 2014

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (kushoto) akimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Rished Bade Ngao ya ushindi wa kwanza kwa taasisi za serikali kwa kuweka kumbukumbu za mahesabu vizuri  mwaka 2013/14 inayotambuliwa na Bodi ya Wakaguzi wa Mahesabu nchini (NBAA), juzi mkoani Arusha, wanaoshudia ni wafanyakazi wa TRA.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akifurahia jambo na Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu
Taasisi za  serikali, mashirika ya umma  wizara na idara  mbalimbali za serikali zimeshauriwa kushiriki katika mashindano ya uwasilishaji wa taarifa bora za fedha za mwaka  tofauti na ilivyo sasa ambapo makundi haya yamekuwa  yakishiriki kwa uchache  sana  na sehemu kubwa ya washiriki  kuachiwa  taasisi na mashirika binafsi. 

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo na vyeti kwa washindi  katika uwasilishaji  wa taarifa bora za fedha mwaka  2014, Naibu Waziri wa Fedha, Adamu Malima  amesema  ni wakati mwafaka  kwa  taasisi na idara mbalimbali za serikali kuingia katika mashindano hayo ili kujipima na kuongeza ufanisi katika utunzaji na uandaaji wa taarifa zao kulingana na viwango vya kimataifa IFRS.


 Katika mshindano hayo ambayo huratibiwa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA kwa mwaka huu  jumla ya washiriki 40 walishiriki  ambapo  mamlaka ya mapato nchini TRA Iliibuka mshindi  wa kwanza kwa uwasilishaji wa taarifa bora za  fedha kwa mwaka 2013 -2014. kwa upande wa taasisi za serikali.

Posted by MROKI On Monday, December 08, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo