Wahitimu wakiwa katika pozi za kusubiri sherehe ya kuwaaga rasmi kutoka elimu ya awali kuingia elimu ya msingi |
Mgeni rasmi wa mahafali hayo mama NEEMA KIBANGA ambaye ni afisa elimu wa kata ya bunju akikabidhi vyeti kwa wahitimu shuleni hapo |
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao baada ya kukabidhiwa vyeti vyao |
Mmoja
wa wamiliki wa shule hiyo ambaye ni mke wa meneja wa shule hiyo BI ROSE
MWALONGO akizungumzas na watoto wa shule hiyo mapema kabla ya kuanza
shughuli rasmi ya mahafali ya shule hiyo
******
|
Shule ya wanafunzi wa awali ya ABEL
MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL leo imefanya mahafali ya wanafunzi wa awali
wanaovuka kuingia elimu ya msingi huku ikiwa na mafanikio makubwa tangu
kuanzishwa kwake shule hiyo mnamo mwaka 2012.
Shule
hiyo ambayo inapatikana BUNJU jijini Dare s salaam ambayo ilianza mwaka 2012
ikiwa na jumla ya watoto tisa tu na mwalimu mmoja ambapo mwaka 2013 idadi
iliongezeka na kufikia watoto 13 na hatimaye mwaka huu wa 2014 shule hiyo ina
watoto 31 pamoja na walimu wawili jambo ambalo limetajwa kuwa ni mafanikio
makubwa kwa shule ya watoto iliyoanzishwa na watanzania wazalendo kwa ajili ya
kuinua elimu ya watoto wa Tanzania.
Akizungumza katika mahafali ya shule hiyo leo meneja
wa shule hiyo Bwana STANSLAUS ABED MWALONGO amesema kuwa lengo lilikuwa ni
kuanzisha shule ya secondary lakini baada ya kutafakari kwa kina akaona ni
vyema kuanzisha shule ya awali na msingi ili kutoa msingi bora wa elimu kwa
watoto wetu.
0 comments:
Post a Comment