Mjane
wa aliyekuwa msanii wa muziki Mzee Gurumo akikabidhiwa hundi ya shilingi
milioni mbili na afisa mahusiano wa NSSF Juma Kintu.
Shirikisho
la Muziki Tanzania, ‘SHIMUTA’ likishirikiana na NSSF wamemkabidhi mjane wa
msanii wa muziki, Mzee Muhidin Maalim Gurumo shilingi milioni mbili kama ahadi
yao waliyoitoa kipindi cha nyuma.
Akizungumza
na waandishi wa habari ndani ukumbi wa Benjamini Mkapa Towers, Rais wa
shirikisho la muziki, Addo November amesema walimuaidi mjane huyo kumpatia
Bajaj ili iweze kumsaidia kimaisha.
“Hapo
mwanzo tulimwaidi mjane tutamnunulia Bajaj ili iweze kumsaidia katika maisha
yake,” alisema. “Leo tumetimiza hili tukishirikiana na wadau wetu NSSF.
Tumefanikisha kutimiza ahadi kwa kumkabidhi mjane cheki ya milioni mbili.
Tumeona tumkabidhi pesa mwenyewe ili ajue kama ataenda kununua Bajaj au pengine
anahitaji mahitaji mengine. Kwahiyo tumeona pesa inaweza kumsaidia zaidi.”
Naye
mjane wa GuRumo alilishukuru shirikisho la muziki pamoja NSSF ambao wameona
umuhimu wa kumsaidia katika kipindi hicho kigumu.
“Nawashuku
wote, nalishukuru shirikisho la muziki pamoja na mfuko wa jamii NSSF kwa
kuniondoa na ukiwa,” alisema.
Rais wa shirikisho la muziki Ado November akizungumza na waandishi wa habari
Mjane mzee Gurumo
Mjane wa Gurumo akipokea hundi
Mmoja kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa band akizungumza
0 comments:
Post a Comment