Na Father Kidevu Blog
Mshitakiwa wa kesi ya kukutwa na dawa za kulevya Abdul Koroma (33) amekufa papo hapo baada ya kupigwa risasi alipokuwa akijaribu kutoroka chini ya ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam.
Mshitakiwa wa kesi ya kukutwa na dawa za kulevya Abdul Koroma (33) amekufa papo hapo baada ya kupigwa risasi alipokuwa akijaribu kutoroka chini ya ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam.
Koroma ambaye ni raia wa
Sierra Leone, alifikishwa mahakamani hapo na kuomba kwenda kujisaidia, akiwa
chooni alivua suluari yake ya jinsi na kuitumia kama ngao ya kujikinga na chupa
zilizoungu ukuta wa choo cha mahakama, akafanikiwa kuruka na kuanza kukimbia.
Kwamujibu wa mashuhuda, askari
magereza alimuona na kuanza kumkimbiza huku akifyatua risasi mbili hewani
kumtahadharisha, lakini aliendelea kukimbia kwa lengo la kuruka uzio wa
Mahakama.
Mlizi wa mahakama hiyo
alijaribu kumzuia kwa kumshika miguu ili asiruke lakini wakati mapambano
yanaendela askari alifyatua risasi iliyompat Koroma ubavuni karibu na kwapa na
kupita hadi kichwani, akaanguka juu ya uzio wa mahakama hiyo.
Koroma alikuwa katika gereza
la Keko, akikabiliwa na kesi namba PI 21 ya mwaka 2013 kwa madai ya kukutwa
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akisafirisha gramu 1229
za dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye thamani ya Sh milioni 61,482,50.
Upande wa Mashitaka katika
kesi hiyo wanasubiri hati ya kifo ili wafute mashitaka dhidi yake na Mwili wa marehemu umehifadhiwa
katikaHospitali ya Taifa ya Muhimbili.
0 comments:
Post a Comment