Nafasi Ya Matangazo

December 22, 2014

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba  akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu, wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), kwa ajili kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamari, katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Buguruni Viziwi jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na (kulia) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abubakar Rakesh na mnufaika wa kibanda hicho, Hebron Mwansele (kwenye baiskeli).
 Sehemu wa wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), wakiwa katika hafla hiyo.
 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikagua kioski baada ya kukabidhi.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwatunza pesa wanamuziki ya walemavu ya Bendi ya Tunawajali, iliyokuwa ikitumbuiza katika hafla hiyo.
*********
Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu yenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali

Sambambal na hilo Airtel pia imewapatia mtaji wa kuanzisha biashara ili  kuwawezesha watakao nufaika na vibanda hivyo kuwa mawakala wa huduma ya Airtel money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Saalam.

Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano , Naibu Waziri wa mawasiliano Mh. Januari Makamba alisema” tunapenda kuwashukuru  Airtel kwa kutanua wigo na kutoa msaada kwa watu wenye ulemavu ili  kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. Serikali yetu iko makini katika kuhakikisha kila mtanzania anapata haki sawa bila kubagua makundi natoa  fulsa sawa katika maeneo mbalimbali.

Sisi kama Serikali tunaamini msaada mliopokea leo utakuwa chachu ya kuleta maendeleo ya kiuchumi na nyenzo kwa wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu kujikwamu na tatizo la kiuchumi unaowakumba makundi mengi kama haya katika jamii”.

Sera ya serikali kwa walemavu inalenga kuboreshea mazingira watu wenye ulemavu na kuwahusisha katika shughuli za uzalishaji ili kuinua uchumi na kutumia kwa ufanisi rasilimali zilizopo katika kuboresha huduma. Naaamini kwa Airtel kuwekeza kwenye jamii leo hakutachangia kuboresha maisha ya wengi tu  bali kutachangia kutekeleza na kutilia mkazo agenda za Serikali.

Nachukua fulsa hii kuwaomba makampuni mengine na wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kutoa misaada ya muda mrefu na endelevu katika makundi mengine kama haya nchini kama ilivyofanywa na Airtel leo”. Aliongeza Makamba

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bibi Beatrice Singano alisema “ kwa mara nyingine tena tumefikia jamii kupitia mpango wetu wa huduma kwa jamii tukiamini kwa kufanya hivi tunachangia na kusaidi familia za wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu , pamoja na kuinua uchumi kwa watu wenye ulemavu kwa ujumla. Airtel tunatoa fulsa na kuwawezesha wale waliokuwa na ndoto za kumiliki biashara zao kuweza kuzifikia ndoto hizo na kujikita kwenye ujasiriamali na biashara. 

Tunaamini Msaada huu haujalenga kuwapatia mtaji tu bali vifaa vya kuendesha biashara pamoja na mafunzo ya jinsi ya kuendesha biashara endelevu.  Tunauhakika ushirikiano tulioanzisha leo utawaweza wanachama wa kikundi hiki kuwa sehemu ya kutoa huduma zetu na hivyo kupata faida itakayowawezesha kuwa wajasiriamali bora nchini’

Tunawaasa wale wote watakaofaidika na msaada huu leo kutumia vibanda hivi kwa ubunifu na kuhakikisha vinawanufaisha kufikia malengo yao ,bado tutaendelea kushirikiana pamoja nanyi na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha tunatimiza lengo letu la kuboresha maisha ya watanzania kupitia huduma na bidhaa zetu za kibunifu na fursa za kibiashara’ aliongeza Singano

Kwa upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu Bw. Abubakar Rakesh alisema” tunayofuraha kuona baadhi ya wenzetu wakiwezeshwa kupata rasilimali muhimu za kuanzisha biashara. 

Tunawashukuru Airtel kwa msaada huo na kwa kukiwezesha kikundi hiki kuwa cha kwanza kupata msaada kama huu . Wito wangu kwa wanachama wenzangu ni kutumia nafasi hii vizuri, kuweka jitihada  katika kazi zao ili kufanya vyema na kufanikiwa katika biashara zao” 

“Napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa serikali na kwa Mh Makamba,kwa mchango wake na kujitolewa kwake  kuwasaidia  watu wenye ulemavu” aliongeza Rakesh
Posted by MROKI On Monday, December 22, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo