Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya Johns
Hopkins (kushoto) na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi (kulia)
muda mfupi baada ya kuwasili ili kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya
Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi
asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika
salama.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward
Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji
uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland
nchini Marekani Jumamosi asubuhi.
*******
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014
Mungu amjaalie afya njema rais wetu apone
ReplyDelete