Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu akiwa amebeba tuzo
aliyokabidhiwa na na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal
(katikati). Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ameukabidhi uongozi wa
Hospitali ya Kairuki (KH) tuzo ya waliofanya vizuri
katika vigezo mbalimbali vya uboreshaji viwango vya huduma ya Afya katika mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji
Viwango vya huduma ya Afya uliofanyika wiki iliyopita (Octoba 31-2014) katika
ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu alisema sifa ya
mafanikio yao mpaka wakapata tuzo hiyo yanatokana na mafunzo kwa
wafanyakazi wa Hospital wapatao 20 yaliyoendeshwa na Wizara ya afya
ikishirikiana na Jhpiego,CDC na PEPFAR.
Dk. Mchomvu aliongeza kuwa mafunzo
kuendelea kutolewa na wakufunzi wa ndani (inhouse training), kuundwa kwa timu
maalum ya ndani kwa ajili kufanya ukaguzi wa kushtukiza ndani na utayari wa KH
kushirikia katika zoezi la udhibiti na uzuiaji wa maambukizi.
Aidha, Dk. Mchomvu alieleza kuwa
siri nyingine ni ushirikiano mzuri baina ya manegimenti ya KH na timu ya
wakaguzi toka wizara ya Afya katika kutekeleza maagizo na mapendekezo na
kuyafanyia kazi.
“Kwa upande wetu maeneo yaliyofanya
vizuri katika zoezi ili ni pamoja na mashine bora za kuuwa vijidudu (sterilization
unit) na eneo zima katika kitengo hicho, eneo la kuifadhi/ kutenganisha na
usafirishaji wa taka hatarishi, taka mbichi na taka mchanganyiko pia chumba cha
upasuaji kufuata taratibu stahiki za kimataifa katika kuzithibiti maambukizi,”
alisema Dk. Mchomvu.
Aliongeza kuwa wakati huohuo KH
imezindua kampeni maalum za muda mrefu katika kuchunguza na kutibu magonjwa
yasiyoambukiza, mfano saratani ya matiti, saratani ya shingo ya kizazi na
saratani ya tezi dume (prostate). Saratani hizi ndizo zinazoongoza kwa
hapa nchini.
“Lakini pia KH imezidi kuboresha huduma
katika vitengo vya macho, sikio, pua na koo kwa kupata mitambo ya kisasa
katika nyanja hizo,” alisema Dk. Mchomvu.
Aliongeza kwa kusema kuwa KH imezindua
wodi mpya ya kisasa hasa kwa ajili ya wanachama wa mfuko wa Bima ya taifa
ya afya. (NHIF) na wodi maalum ya watoto.
Wengine waliotunukiwa tuzo hizo za
uboreshaji wa huduma za afya ni Hospitali ya Bugando-Mwanza pamoja na Kilimanjaro
Christian Medical Centre (KCMC).
Tuzo
hizo zilitolewa na Wizara ya Afya wakishirikiana na Kituo cha Kudhibiti Maradhi
cha Marekani (CDC) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na
UKIMWI (PEPFAR).
0 comments:
Post a Comment