Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012,Bi.
Brigitte Alfred akimtumza mmoja wa vijana wenye ulemavu wa ngozi
(albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo,aliekuwa akighani shairi
alilolitunga,wakati wa hafla ya kusherehekea Mafanikio ya Vijana hao
iliyofanyika leo kwenye Viwanja Makumbusho,Jijini Dar es Salaam.Taasisi
ya BAF kupitia Mpango wake wa JA (Juniour Achievement) imeweza
kuelimisha vijana 50 wenye ulemavu wa ngozi katika mpango wa kutoa elimu
ya kujitambua, ujasiriamali na stadi za biashara ili waweze kuthubutu,
kuanzisha na kuendeleza biashara na shughuli nyingine za kiuchumi
zitakazo wapa ajira, kipato na kuinua ustawi wa maisha yao na familia
zao.
Kijana mwenye ulemavu wa ngozi (albino) akighani mashairi yake.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012, Bi.
Brigitte Alfred akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Pugu waliofika kwenye hafla hiyo ya kusherehekea
Mafanikio ya Vijana,yaliyofanyika leo kwenye Viwanja Makumbusho,Jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation),Bi.
Brigitte Alfred akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana wenye
ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo.
Baadhi ya Wanahabari waliohudhulia hafla hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na
Miss Tanzania 2012,Bi. Brigitte Alfred pamoja na baadhi ya vijana wenye
ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo. SOURCE: MICHUZI MEDIA.
0 comments:
Post a Comment