Na Fadher Kidevu Blog
KLABU 14 zinazoshiriki Ligi
Kuu Tanzania Bara zimetishia kutotumia
jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu
wa ligi ambaye ni Vodacom pamoja na matangazo ya moja kwa moja ya Azam Televisheni
endapo Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania TFF itakata asilimia
tano ya mgawo wa fedha za udhamini kama
ilivyoaga.
Wakili anayezisemea klabu hizo
Damasi Ndumbaro ameiambia Goal kwamba klabu hazina imani na Rais wa TFF Jamal
Malinzi na kutaka kuitishwa mkutano mkuu wa dharura na kumwomba Mkaguzi Mkuu wa
Serikali kufanya ukaguzi TFF ili kuangalia
matumizi mabaya ya fedha.
Alisema atakayethubutu kukata
makato hayo watasimamisha Ligi siku ya pili, na kutotumia vifaahivyo muhimu na
katika kutekeleza hilo watawaandikia barua wadhamini hao Vodacom na Azam
Televisheni kuwajulisha kinachoendelea.
Dk. Ndumbaro alisema kitendo
cha Malinzi kusema Bodi ya Ligi sio chombo huru ni upotoshwaji, na kwamba ukweli
kile ni chombo huru kama ilivyo
Kamati ya Sheria na nidhamu na kwa mujibu
ibara ya 40 kifungu kidogo cha (1) kitendo cha TFF na Kamati ya Utendaji
kuingilia mamlaka ya Bodi ni ukiukwaji, mwenye mamlaka ni Mkutano Mkuu.
Alifafanua kuwa Kamati ya Mashindano ya TFF ndio yenye
mamlaka ya kuandaa kanuni na ndio waliopendekeza asilimia tano na sio Kamati ya
Utendaji kama alivyobainisha Malinzi.
Pamoja na hilo, alisema Rais
huyo amepotosha kuwa Bodi ya Ligi haina mamlaka ya kusaini
mikataba ya wadhamini kisheria wakati katika mkataba wa Azam wa mwaka 2013 kuna sahihi ya TPL, TFF na Azam
Media na kuongeza kuwa mkataba ambao Malinzi aliowaonyesha waandishi wa habari
ni wa mwaka 2012 ambapo Bodi hiyo ilikuwa haijaundwa.
Juzi Malinzi alisema watake
wasitake lazima makato hayo yakatwe kwa
ajili ya kusaidia maendeleo ya soka la vijana.
0 comments:
Post a Comment