Meneja
wa uendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah
Mbena akikabidhi rasmi moja kati ya makasha matatu ya kuhifadhia taka
yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya. Kulia ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.
Baadhi
ya michoro iliyopo kwenye majengo ya shule ya msingi Bunge
yanayohamasisha utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Wanafunzi wa klabu ya mazingira shule ya msingi Bunge wakiagana na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.
**********
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Usafi ya Green Waste Pro imetimiza ahadi yake ya kuipatia shule ya
Msingi Bunge makasha ya kuhifadhia taka na vifaa vya usafi wa mazingira
iliyoitoa mwaka jana.
Mwaka
jana wakati wanafanya shughuli ya kupaka rangi shule hiyo,kampuni hiyo
ilifurahishwa na mazingira ya shule jinsi yanavyotunzwa kiasi cha
kufanya maamuzi ya kuwapelekea vifaa vya mazingira na hasa makasha ya
kuhifadhia taka.
Kwa
mujibu wa Afisa uendeshaji wa kampuni hiyo Abdallah Mbena,ambaye ndiye
aliyekabidhi makasha hayo,maamuzi ya kuwapatia makasha yametokana na
jinsi klabu ya mazingira ya shule hiyo na mwalimu wao anavyochakarika
katika kuhakikisha usafi wa mazingira katika shule hiyo.
Mbena
alisema kwamba wamefarijika sana na juhudi zinazofanywa na mwalimu na
wanafunzi wake katika kuhakikisha kwamba wanatunza mazingira.
Pamoja
na sababu za wanafunzi hao na mwalimu wao katika kutoa kipaumbele
mazingira, kuwa chanzo cha kutolewa kwa makasha hayo, sababu nyingine
iliyozingatiwa ni kuwa shule hiyo ipo katika kata ya Kivukoni ambapo
kampuni hiyo inazabuni ya kufanya usafi.
Amesema
wana mpango wa kuwapatia vifaa vya aina hiyo kwa shule nyingine
zinazofanya vyema kwenye usafi wa mazingira ila kwa sasa wameanza na
shule ya Bunge.
Mwalimu
wa mazingira wa shule hiyo, Frida Madanganya ameshukuru kampuni hiyo
kwa kuendelea kuwasaidia na anawategemea wataendelea zaidi kuhakikisha
kwamba shule hiyo inakuwa namba moja kwa utunzaji wa mazingira.
Naye
Mwalimu Mkuu Khadija Telela alisema shule yake ina changamoto kubwa
hasa maji ya Dawasco kwani maji yao ni yachumvi kwa kisima
walichochimba.
0 comments:
Post a Comment