Na
Fadher Kidevu Blog
WASHINDI
wa Ngao ya Jamii msimu wa 2014/2015 timu
ya Yanga inaondoka leo asubuhi kuelekea
Morogoro tayari kwa mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
dhidi ya wakata miwa Mtibwa Sugar katika dimba la Jamhuri.
Yanga
chini ya Mbrazil Marcio Maximo imepania kuhakaikisha safari hii inavunja mwiko
wa kukosa ushindi katika dimba la Jamhuri kwa takribani miaka minne mfululizo,
na maandalizi ya mchezo yanakwenda vizuri na wachezaji wote wapo fiti ispokuwa kiungo
Mbrazili Andrey Coutinho.
Aidha
Maximo amesema anatambua Mtibwa Sugar wana kikosi kizuri ambacho kimekaa pamoja
kwa muda mrefu, baadhi ya wachezaji aliwahi kuwafundisha akiwa kocha wa timu ya
Taifa Taifa Stars Mecky Mexime ambaye
kwa sasa ni kocha wa wana Tamtam hao.
"Natambua
ugumu uliopo kwenye mchezo wa Jumamosi lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata
ushindi Mtibwa nitimu nzuri na watakua
nyumbani sikuhiyo wakihitaji pointi tatu lakini hata sisi tunakwenda Morogoro
kuhakikisha tunavunja mwiko na kurudi na pointi zote tatu”anasema Maximo.
Kuhusu
maendeleo ya mchezaji Andrey Coutinho na Jerson Tegete wanaendelea vizuri na
mazoezi lakini daktari ameona wabakie jijini Dar es salaam wakiendelea na
programu nyingine chini ya usimamizi wa madaktari wa timi huyo
Kikosi
cha wachezaji watakaoondoka kesho asubuhi
Makipa ni:
Deo Munishi "Dida", Juma Kaseja na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir,
Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Mbuyu Twite, Omega Seme, Hassan
Dilunga, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima na Said Juma "Makapu"
Washambuliaji: Said Bahanuzi, Hussein Javu, Hamis
Kizza, Geilson Santos "Jaja", Saimon Msuva na Mrisho Ngasa
0 comments:
Post a Comment