Mbunge wa Nzega ambaye pia ni Mchezaji wa timu ya wabunge wa Simba, Dk. Hamis Kingwangala (kushoto) akiwa uwanjani akilisakata kabumbu.
*******
Wakati nafanya tafakuri ya kama nigombee Urais mwakani ama la,
haikunitokea hata siku moja kutamani kuutumia ujana wangu kama silaha ya
kutafuta comparative advantage over wazee ukizingatia zaidi ya asilimia
60 ya population yetu ni vijana.
Sababu kubwa iliyoniijia haraka haraka
ni kuwa ujana pekee haitoshi kuwa kigezo cha mtu kuchagulika kuwa Rais
ama haitoshi kuwa sifa ya kumnyima mtu fursa ya kuwa Rais; kwangu mimi
Urais ni nafasi anayopaswa kupewa ama kunyimwa mtu kwa uwezo
wake, sifa zake, rekodi yake n.k. Pia nimekuwa nikijiuliza kama ukipiga
jalamba leo kuwa Rais wa sasa ni lazima awe kijana, hivi usipochaguliwa
mpaka ukazeeka ndiyo kusema utaacha kugombea sasa?
Nimepata fursa ya kusoma habari kwenye gazeti la Nipashe kuwa 'Urais si lelemama.' Humo amenukuliwa Dkt. Hassy Kitine, akisema wanaotaka Urais na wakatangaza nia ndiyo kwanza wamepoteza sifa ya kuwa Rais na watazamwe, kauli iliyokuja baada ya mimi kutangaza nia majuzi;
Dr. Kitine anasema kuwa Urais ni nafasi ambayo
unapaswa kuambiwa na wengine kuwa unauweza na hivyo kushawishiwa
ugombee.
Hapa nikaona kumbe ile hoja ya baadhi ya vijana wenzangu kuwa
'wanaona ni kitu kigumu kukubali kuongozwa na watu wa kizazi kingine
ambao hawatakuwepo miaka 30 ijayo' inapaswa kufanyiwa tafakuri sana.
Maana Dr. Kitine anatoa mfano namna Rais Mwinyi na Rais Mkapa
walivyopatikana, na anaona kama hiyo ndiyo 'gold standard' ya kupata
Rais bora kabisa.
Ninachokiona hapa ni mwendelezo wa kuamini mambo
mazuri ni yale ya kizazi chako tu, mapya yote ni mabaya na hayafai! Mimi
na wenzangu tunaoamini katika mapinduzi ya kifikra tunadhani tunahitaji
kufanya mambo kwa utofauti ili tutoe matokeo tofauti. Haijalishi
matokeo yatakuwaje, mazuri ama mabaya. Tofauti tu. Thats the key
word.
Maana miongoni mwetu wanamabadiliko ya kifikra tunaamini kwamba kama
unataka nafasi ya Urais usijifiche, we sema ili tukupime. Na kwamba
kumwambia mtu ana uwezo na Urais ni kumkurupusha tu. Anaweza akawa hana
vision wala agenda yoyote kwa nchi.
Ni vema akasema anataka Urais na
tukamhoji ana vision gani. Ili tushindanishe agenda za kila anayetamani.
0 comments:
Post a Comment