Meneja
wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia),
akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi
milioni 4.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mwakilishi wa
Afisa Elimu ya Sekondari Manispaa ya Temeke, Yasintha Kayoza kwa niaba
ya shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla
iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam
jana. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu
Marcelina Kimario.
Meneja
wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani),
akiangalia moja ya vitabu vya masomo ya sayansi baada ya kuvikabidhi
vitabu vyenye thamani ya milioni 4.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule
Yetu’ kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika
hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es
Salaam jana.
Meneja
wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia),
akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 1.5/-,
kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario katika hafla iliyofanyika shuleni
hapo jijini Dar es Salaam jana. Sekondari nyingine zilizokabidhiwa
vitabu hivyo ni pamoja na Mvuti na Kambangwa. Kushoto ni Mwakilishi wa
Shule ya Sekondari Kambangwa, Mwalimu Sueiba Mfinanga.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Mbagala wakifurahia vitabu vya masomo ya
sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa ‘Shule Yetu’
kukabidhi vitabu hivyo vyenye thamani ya milioni 4.5/- kwa shule tatu za
sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika
shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.
*********
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa “shule yetu”
umeendelea na mpango wake wa kuchangia katika kusaidia sekta ya elimu
nchini ambapo leo imetoa msaada wa vitabu kwa shule 3 za sekondari
jijini Dar es saalam
Shule
zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na Kambagwa sekondari iliyopo
wilaya Kinondoni, shule ya sekondari Mvuti iliyopo wilaya ya Ilala na
shule ya sekondari Mbagala iliyopo wilaya ya Temeke ambapo kila shule
imepata vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.
Akiongea
wakati wa kukabithi vitabu hivyo, Meneja huduma kwa jamii Airtel Bi
Hawa Bayumi alisema” Tunayofuraha kuendelea na mpango huu wa “shule
yetu” kwa mwaka huu na kuwa na shule mpya zitakazofaidika na vitabu vya
masomo ya Sayansi. Tunazo shule zaidi ya 30 ambazo tumezipata kwa
kushirikiana na uongozi wa serikali zitakazofaidika na msaada huu wa
vitabu kwa mwaka huu, Na leo tumeweza kuzifikia shule za Kambagwa, Mvuti
na Mbagala na kuwapati vitabu vitakavyoweza kuleta tija katika ufaulu
na elimu kwa ujumla”.
“Nia
yetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu
katika kuinua sekta ya elimu nchini huku tukiwekea mkazo katika masomo
ya sayansi kwani tuaamini ulimwengu na nchi inahitaji wanasayansi wengi
ili kwenda na kasi ya ukuaji wa technologia. natoa wito kwa walimu na
wanafunzi basi watumie vitabu vizuri na kuweza kuongeza wanafunzi wengi
katika masomo ya sayansi na hatimae kuongeza ufaulu zaidi.aliongeza”
Bayumi
Akiongea
kwa niaba ya walimu wakuu wa shule zilizopokea msaada jijini Dar es
saalam, Mwalimu mkuu wa shule ya Mbagala Bi Marcelina Kimaro alisema”
Tunawashukuru sana Airtel kwa kutufikia leo, tumekuwa tukiona shule
nyingi zikifaidiaka na mpango huu wa “Shule yetu” na leo tunayofuraha
kupokea msaada wa vitabu vya Hisabati, Chemia, physikia na Baiologia
kutoka Airtel
Shule
hii ya mbagala Sekondari ina jumla ya wanafunzi 2031 na uwiano wa vitabu
kwa wanafunzi kwa sasa ni kati ya kitabu kimoja kwa wanafunzi wa 3 au 4
, kwa msaada huu leo utasaidia kupunguza changamoto tuliyonayo ya uhaba
wa vitabu na kufanya uwiano kuwa kitabu kimoja kwa wanafunzi wawili.
Halikadhalika msaada huu utatupatia urahisi katika kusoma na walimu
kuandaa masomo yao.
Kimaro
aliongeza kwa kusema” Vitabu hivi vimetupa changamoto kubwa ya kuongeza
juhudi katika masomo kwani nyenzo sasa tunazo na tunaamini wanafunzi
wetu wa masomo ya sayansi watasoma kirahisi na hatimaye kupata idadi
kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi. Tunawaahidi kuvitunza na
kuvitumia vitabu hivi kwa faida ya wanafunzi na jamii kwa ujumla”
Chini
ya mpango wa “shule yetu” Airtel imeweza kutoa msaada wa vitabu kwa
shule za sekondari zaidi ya 1000 nchini huku mpango ukiwa ni kizifikia
shule nyingi zaidi kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment