Meneja
wa bia ya ndovu special Malt Bi Pamela Kikuli
kulia akikabidhi baadhi ya vifaa mbalimbali vya kusaidia kupambana na
ujangili wa mauwaji wa Tembo nchini. Anaepokea ni katikati ni mkuu wa kitengo
cha Ulinzi na upambanaji wa Ujangili toka hifadhi ya Serengeti Ndugu Agrikola
Luhiru na kushoto ni meneja Mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete
Meneja
Mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari wakati
akipokea vifaa vya kupambana na ujangili wa Tembo toka kwa bia ya Ndovu special
Malt ambavyo ni Trimble GPS na Darubini (Binoculars) Kulia ni Meneja wa bia ya
Ndovu Special Malt Pamela kikuli.
Bia
maarufu ya Ndovu Special Malt leo imefungua ukurasa mwingine ikiwa ni
muendelezo wa harakati zake za kusaidia kuimarisha ulinzi wa Tembo wetu hapa
nchini. Bia hii ya Ndovu Special Malt ambayo pia imebeba jina la mnyama huyu
adhimu “Ndovu” anayekabiliwa na tishio kubwa la kutoweka duniani kufuatia
uwindaji haramu na ujangili uliokithiri, imedhamiria kufanya kila
linalowezekana katika kumlinda mnyama huyu.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari jijini dar es salaam, meneja wa bia ya
Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema; Bia ya Ndovu Special Malt imeweka mikakati na
dhamira kubwa kuhakikisha tunamlinda mnyama huyu Tembo kwa njia yoyote ile. Huu
ni urithi wetu na vizazi vijavyo, na pia ni fahari ya Taifa letu kama ilivyo
bia hii ya Ndovu, hivyo tukiacha mnyama huyu akatoweka tutapoteza fahari ya
taifa letu na urithi wetu. Kwa kulitambua hilo, Bia ya Ndovu imeamua kuwa
mstari wa mbele kuhakikisha Tembo wetu wanalindwa kwa kila itakavyowezekana.
Kama
mtakumbuka mwaka jana bia ya Ndovu iliendesha kampeni ya kumlinda tembo dhidi
ya majangiri kupitia mitandao ya kijamii na kuwazawadia watu walioshiriki
katika kampeni hiyo zawadi ya kwenda kujionea makundi ya Tembo katika hifadhi
ya Selou na kusaidia Asasi moja inayojihusisha na ulinzi wa Tembo. Mwaka huu
tumekwenda mbali zaidi na kuamua kutoa vifaa muhimu kabisa vinavyosaidia katika
ulinzi wa Tembo wetu, tunatoa viona mbali au Darubini (Binoculars) 20 na vifaa makini
vya utambuzi wa mahala walipo tembo (Trimble GPS) 5, ili kuimarisha doria dhidi
ya majangiri hawa. Tuna imani kubwa kuwa vifaa hivi vitasaidia sana katika
ulinzi wa Tembo wetu na hivyo kutimiza malengo yetu. Alisema Pamela.
Akiongelea juu ya
hatari inayolikumba taifa letu kwa jinsi Tembo wanavyoteketea kwa kasi Pamela
alisema; TBL tumeona jinsi Tembo wetu wanavyoteketea kwa kasi hapa Tanzania na
Afrika kwa ujumla, ili kuokoa hali hii tukaipa jukumu Bia yetu iliyobeba jina
hili lenye ufahari wa pekee, bia ya Ndovu kuchukua jukumu la ulinzi wa myama
huyu. Katika kutekeleza hayo tunawashirikisha wananchi na wapenzi wa bia hii
katika zoezi hili kupitia mitandao ya kijamii. Mwaka huu tumeshirikiana na
uongozi wa TANAPA na wenzetu wa Serengeti National Park kuona ni jinsi gani
tutaimarisha doria katika hifadhi zetu. Na tunaahidi kuwa kampeni hii ni
endelevu hadi tuhakikishe mafanikio yamepatikana.
Nae Meneja Uhusiano wa Tanapa Bw. Pascal Shelutete
alisema; TBL kupitia bia yake hii ya Ndovu Special Malt, imekuwa mstari wa
mbele katika ulinzi wa Tembo wetu. Wote sisi ni mashuhuda wa mchango ambao Bia
ya Ndovu inautoa katika kuhakikisha
Tembo wetu wanakuwa salama, lakini pia kuwahamasisha watanzania wengine kujenga
dhamira ya kuwalinda wanyama hawa wakubwa, wapole na wa kuvutia. Vifaa
walivyotupatia leo, ni miongoni mwa vifaa muhimu sana katika ulinzi wa wanyama
wetu. Hivyo tunawashukuru sana na kuomba waendelee na moyo wao huu wa
kizalendo. Nichukue nafasi hii pia kuwaomba makampuni na taasisi nyingine kuiga
mfano huu bora wa TBL.
Nae mkuu wa kitengo cha kudhibiti ujangili toka hifadhi
ya Serengeti, Bw. Agrikola Luhiru alisema; vifaa hivi ni muhimu sana katika
doria zetu, vinarahisisha kazi yetu na kutupa uwezo wa kutambua walipo tembo
muda wowote na kuweza kuwafuatilia kwa umakini. Lakini pia kuwaona majangiri
hata kama watakuwa umbali mrefu na kuwadhibiti. Tunaahidi kuvitumia vifaa hivi
kwa malengo yaliyokusudiwa na si
vinginevyo. Nami napenda niongeze shukurani zangu za dhati kwa niaba ya hifadhi
ya Serengeti kwa wenzetu hawa wa Ndovu Special Malt kwa dhamira hii nzuri ya
kulinda Tembo wetu. Alisema Luhiru.
0 comments:
Post a Comment