Na Fadher Kidev Blog
MSHAMBULIAJI Didier Kavumbagu ameifungia Azam
mabao mawili na kuipa ushindi wa 2,mfululizo katika Ligi Kuu ya Tanzania bara.
Kavumbagu aliyejiunga na Azam msimu huu akitokea
Yanga, amefikisha mabao manne katika mechi mbili za ligi ya msimu huu
alizoichezea timu hiyo.
Katika mechi ya kwanza dhidi ya Polisi
Moro,Kavumbagu alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1, iliyoupata Azam.
Kavumbagu alifunga bao la kwanza katika dakika
ya 39,akimalizia mpira uliopigwa na beki Shomari Kapombe na kurudi uwanjani
ambao ulimkuta na kuukwamisha wavuni.
Ilimchukua dakika tano za kipindi cha pili
Kavumbagu kuifungia Azam bao la pili na kuwaacha wapinzani wao Ruvu Shooting
wanaofundishwa na kocha Tom Olaba wakianza vibaya msimu huu kwa kupoteza mechi
zote mbili za awali ikiwemo ile ya kwanza dhidi ya Prisons.
Katika mechi hiyo washambulaji wa Ruvu Shooting
walionekana kukosa kabisa mbinu za kuipita beki ya Azam angalau kupata bao moja
Angalau mshambuliaji mpya wa timu hiyo Chagu Faustine dakika ya 25 alipata
nafasi akiwa nje ya 18 lakini shuti lake halikuweza kulenga lango la Azam
ambalo lilikuwa linalindwa na Aishi Manula.
0 comments:
Post a Comment