Nafasi Ya Matangazo

August 25, 2014

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akisimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
Mwigulu Nchemba akizingumza na umati wa watu katika viwanja vya mwembetogwa mwishoni mwa wiki mjini Iringa
MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akizungumza na Wananchi mwishoni mwa wiki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
 Salim Abri Asas akiwa na Wazee wa Kimila kabla ya kusimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano.
 Shughuli za kusimikwa zikiendelea huku wanahabari wakiendelea kurekodi tukio hilo.
Na Denis Mlowe,Iringa
MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas mwishoni mwa wiki amesimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.

 Akimuapisha Asas kuwa Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisema analitumikia taifa hili akijua sehemu kubwa ya wananchi wake ni masikini na lengo kubwa ni kuwaondoa katika lindi la umaskini.

Nchemba alisema nchi inaliwa na moja ya eneo linalowaweka katika kazi kubwa ya mapambano ni fedha zinazotolewa kwenye halmashauri kwa ajili ya maendeleo ambazo hazitumiki ipasavyo na watendaji kwa kuzitumia katika miradi isiyo endelevu na kusababishia nchi kutokuwa na maendeleo.

“Kuna mambo mengi yanatokea katika halmashauri zetu kwasababu ya kukosa usimamizi unaosababisha watu wetu wakose hali ya kupata huduma zinazotakiwa kutekelezwa katika miradi ya maendeleo hivyo nitahakikisha kuwabana na kuwafuatilia kwa kila halmashauri kuleta mchanganuo wa fedha jinsi zilivyotumika na kuhakikisha mradi umekamilika na sio kusema kiasi Fulani kimetumika.”  Alisema Nchemba.
 
Aliongeza kuwa serikali inaendelea na mikakati ya kuwasaka, kuwakamata na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya dola watumishi wa umma wanaokula kodi za wananchi kwa mikono miwili bila kunawa.

Mwigulu alisema mambo mazuri yanakuja na serikali itaendelea kutengeneza sera  zinazojali watanzania ili keki ya taifa iliwe na watanzania wote na kudhibiti matumizi ya ovyo na fedha tutakazokuwa tunatoa hatutaruhusu zitumike kwa kazi tofauti na ile iliyokusudiwa.

Akimpongeza Asas kwa kuwa kamanda wa UVCCM, Alisema UVCCM wakitimiza wajibu wao ipasavyo watasaidia kupunguza maadui wakubwa wawili wa CCM ambao wameendelea kuwa na athari kubwa wakati wa chaguzi za serikali.

Aliwataja maadui hao kuwa ni pamoja na kujiingiza kwenye makundi ya wagombea na hila zinazosababisha baadhi ya wana CCM wasitendewe haki stahiki kwenye vikao muhimu vya chama.

Kwa upande wake Kamanda Salim Asas alisema baada ya kuapishwa kwa kipindi kingine lengo ni kuwainua vijana kiuchumi na kutaka ushirikiano katika kuleta maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa bila kujali itikadi ya vyama na dini.
Posted by MROKI On Monday, August 25, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo