Brigedia
Jenarali Rogastian Shaban Laswai akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusiana na maendeleo ya
ukarabati wa Kivuko cha Mv Kigamboni. Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa.
Luteni
Kanali Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi
Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu uboreshaji wa sehemu ya kupoozea injini ya
kivuko cha Mv Kigamboni.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe ameelezea kuridhishwa
kwake na kazi ya ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni unaoendelea chini
ya kikosi cha Ufundi cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kitengo cha
Wanamaji uliofikia asilimia 40 ya matengenezo yake.
Akizungumza
mara baada ya Ukaguzi huo wa kushtukiza, Mhandisi Iyombe amekipongeza
Kikosi hicho cha Wanamaji kwa kufanya kazi kwa kiwango cha juu na haraka
hivyo kuwa na matumaini ya kukamilika kwa kazi hiyo kwa muda mfupi ili
kuondoa msongamano unaowakabili wananchi kwa sasa.
“Nia
ya Serikali ni kuhakikisha kuwa Kivuko hiki kinakuwa katika ubora
unaokubalika ili kulinda usalama wa abiria na mali katika huduma ya
usafiri huu wa kila siku na unaotegemewa na wakazi wengi wa Kigamboni na
maeneo jirani” Alisema Katibu Mkuu Mhandisi Iyombe.
Aidha,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi amewaomba wananchi kuwa wavumilivu
katika kipindi hiki kifupi cha ukarabati na kuahidi kuwa mnamo Septemba
7, Kivuko hicho kitaanza kazi zake kama kawaida.
“Kutokana
na ukarabati unavyoendelea ni matumaini yangu kuwa kazi hii itakamilika
kwa muda mlionieleza na itakuwa ya kiwango cha juu”. Katibu Mkuu
alisema.
Mhandisi
Iyombe aliahidi kutembelea tena katika Kivuko hicho mnamo mwanzoni mwa
mwezi Septemba mara baada ya kukamilika kwake. Kwa upande wa Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Marceline Magessa
amesema kuwa hadi sasa ukarabati wa MV. Kigamboni upo katika hatua za
marekebisho mbalimbali ikwemo utoaji kutu, kupaka rangi, usafi na
uzibajji wa matundu pembezoni mwa kivuko hicho.
Nae
Mkuu wa Jeshi la Wanamaji Tanzania Brigedia Jenerali Rogastian Shaban
Laswai amafafanua ingawa kuna cha changamoto ya kina cha maji
kinachokwamisha matengenezo ya Kivuko hicho bado wanaamini na
wanajipanga kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba Septemba 7
kivuko hicho kitashushwa kwenye maji.
Ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni chenye uwezo wa kubeba tani 160 na abiria 800 kwa wakati mmoja ulianza Agosti 14 mwaka huu.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wapili kutoka kulia
akipita kukagua matengenezo yanayoendelea ya Kivuko cha MV Kigamboni.
Kulia kwake mwenye kofia ya njano ni Dkt. Wiliam Nsahama Mkurugenzi wa
Huduma za Ufundi (DTES) kutoka Wizara ya Ujenzi.
0 comments:
Post a Comment