Mkuu wa Morogoro Joel Bendera akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoani Morogoro.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akikagua timu wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoani Morogoro.
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera, atilia mkazo soka la vijana na
kuwataka viongozi wa mpira wa miguu mkoa wa Morogoro na chama cha mpira
wa miguu Tanzania kutilia mkazo program za vijana.
Kocha
wa zamani wa timu ya Taifa – Taifa Stars atoa changamoto wakati
akifungua mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel
Rising Stars mkoa wa Morogoro siku ya jumanne. Alisema kuwa hakuna njia
ya mkato katika maendeleo ya mpira wa miguu zaidi ya kuwekeza katika
shule za soka na programu za vijana kama Airtel Rising Stars.
Awapongeza Airtel kwa mchango wao.
Zaidi
ya majuma mawili kumekua na maoni ya kutoka kwa wakuu wa mikoa na wadau
wengine wakisisitiza viongozi wa mpira wa miguu nchini kutilia mkazo
programu za vijana kuiwezesha Tanzania kufanya vizuri.
Wakifungua
mashindano ya Airtel Rising Stars katika mikoa yao hivi karibuni, Mkuu
wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Said Meck Sadiki na Mkuu wa mkoa Mbeya Abbas
Kandoro nao walitilia mkazo kuwekeza katika mpira wa vijana. Wengine
waliotoa maoni hayo ni meya wa Mwanza Stanslaus Mabula na Mbunge wa
Ukonga Eugen Mwaiposa.
Mashindano
ya Airtel Rising Stars yanaitimishwa leo (August 7) na timu
zinatarajiwa kuwasili jijini Dar-es-Salaam siku ya jumamosi August 9
katika fainali za taifa ambazo zinaanza kutimua vumbi jumapili katika
kiwanja cha kumbukumbu ya Karume. Fainali
za Taifa zitamalizika tarehe 17 August na wachezaji wakiume na wa kike
watakao chaguliwa wataweka kambi jijini Dar-es-Salaam wakijiandaa na
mashindano ya kimataifa Airtel Rising Stars yatakayofanyika nchini
Gabon.
Mwaka
jana mashindano hayo yalifanyika nchini Nigeria na timu ya wasichana ya
Tanzania walinyakua ubingwa na kuzawadiwa dollar za marekani 10,000.
0 comments:
Post a Comment