Timu
ya Airtel wakiongozwa na Emanuel Rafael zone Businnes Manager mara
baada ya uzinduzi wa mnara wa kampuni ya mawasiliano ya airtel katika
kijiji cha Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma hafla ya uzinduzi
imefanyika jana kijijini humo
Mkuu
wa wilaya Khadija Nyembo akiongea wakati wa uzinduzi wa mnara wa airtel
katika kijiji cha Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani kigoma hafla ya
uzinduzi imefanyika jana kijijini humi
Kikundi cha Ngoma kikiburudisha katika sherehe za uzinduzi wa mnara wa Airtel kijiji SIGUNGA wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
**********
Yazindua
mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Sigunga mkoani Kigoma,
wanakijiji Kunufaidika na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi toka
Airtel.
Kampuni
ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua rasmi huduma za mawasiliano
katika kijiji cha Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma
Uzinduzi
huo unafatia jitihada za kampuni ya Airtel kuendelea kuboresha
mawasiliano ya huduma za simu za mkononi katika maeneo mbalimbali nchini
husasani katika maeneo ya vijijini huku lengo likiwa ni kuzifikia jamii
zinayoishi pembezoni mwa nchi huduma bora ya Airtel Money.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano Sigunga, Meneja Mauzo
kanda ya Ziwa bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel inatambua adha
wanayoipata wakazi wa kijiji cha Sigunga na maeneo ya jirani katika
kupata huduma za mawasiliano kwa muda mrefu sasa, hivyo tumeonelea ni
vyema basi tukachukua hatua ya kuboresha huduma hizi muhimu kwa
kuwafikishia wanakijiji hawa mawasiliano yatakayowawezesha kufanya
shughuli zao za kila siku kwa ufanisi zaidi
Kupitia
mnara huu sasa tunaweza kuwaunganisha wanakijiji hawa na maeneo mengine
ya nchi, tutawawezesha kupata masoko ya kuuza biashara zao kwa urahisi,
tumewawezesha kupata huduma za kifedha kupitia huduma yetu ya Airtel
Money ambapo sasa wataweza kupokea na kutuma pesa kwa ndugu jamaa na
marafiki pia kupokea malipo ya biashara zao na kuweza kufanya malipo
mbalimbali ya huduma muhimu wakiwa majumbani mwao. Sambamba na hilo
mawasiliano jijini hapa yamekuwa chachu ya maendeleo na ukuaji wa
shughuli za kiuchumi kwa ujumla.
Kwa
upande mkuu wa wilaya ya Uvinza Khadija Nyembo alisema” Tunawashukuru
sana Airtel kwakutambua kwa vitendo umuhimu wa mawasiliano kwa
kutufikishia mawasiliano kijijini hapa. Kupitia mawasiliano ya Airtel
tumeweza kuboresha usalama wa raia na mali zao, kuwezesha kufanyika kwa
shughuli za kiuchumi kiufani , wakulima sasa wanauhakika wa kupata
masoko na kupata malipo kwa kupitia simu ya mkonono. sambamba na hilo
mawasiliano hayo yamewezesha huduma muhimu za kijamii kuboreshwa zaidi.
Natoa wito kwa wakazi wa Sigunga Na vijiji vya jirani kutumia mawasiliano haya katika kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla.
Wakiongea
kwa wakati tofauti wakazi wa Sigunga wameishukuru Airtel kwa
kuwafikishia mawasiliano hayo nakusema , tumekuwa na adha kubwa ya
huduma za simu kabla ya mawasiliano haya kufikishwa kijijini hapa lakini
kwa sasa kero hiyo imekwisha kabisa hivyo tunaipongeza sana kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel kwa juhudi zao.
0 comments:
Post a Comment