Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya banda lao na nyuso za bashasha baada ya kunyakua tuzo ya Machapisho kwa Umma (Mass Media na Publicity) kwa mara ya tatu mfululizo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kutoka kushoto ni Programme Coordination Specialist wa UNAIDS, Jimmy Mbazi, Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, Programme Officer wa Shirika la Kimataifa linalohusika na uhamiaji (IOM), Charles Mkude na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa wameshikilia tuzo pamoja na cheti walichotunikiwa jana wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyopewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama (wa tatu kushoto) akizungumza na mzazi aliyeambatana na watoto wake kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwa ajili ya kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini. Kushoto ni Amos Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana " Kazi Njenje" na anayefuatia ni Programme Coordination Specialist wa UNAIDS, Jimmy Mbazi.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwa mzazi aliyeambatana na watoto kwenye banda la Umoja wa Mataifa kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Mataifa hapa nchini kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Amos Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana "Kazi Njenje" akieleza kwa mmoja wa wadau namna anavyofanya kazi zake za uchoraji ambapo UN imempa nafasi ya kuonyesha kuonyesha kazi zake za sanaa ya uchoraji kwenye banda hilo kwa ajili yakujitafutia soko na kuendeleza maisha yake.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa wageni waliofika kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment