Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akizungumza na wafanyabiashara wa mnadani Mkoani Rukwa mapema leo tarehe 14/07/2014 katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Wafanyabiashara hao waliomba kuonana na Mkuu huyo wa Mkoa kumueleza kero zao ikiwemo tukio la hivi karibuni la tarehe 11/07/2014 la kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kupelekea wafanyabiashara tisini (90) kuporwa simu na fedha katika njia ya Muze. Wafanyabishara hao wamemuomba Mkuu huyo wa Mkoa kuwasaidia katika ulinzi kwenye biashara zao kwani mitaji mingi waliyonayo ni fedha za kukopa ambazo zinahitaji marejesho.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya baada ya kupokea kero za wafanyabiashara hao wa mnadani (hawapo pichani) amelitaka jeshi la Polisi Mkoani Rukwa kuandaa utaratibu maalum wa kuwasaidia wafanyabiashara hao ikiwemo kuwapatia mafunzo maalumu ya mgambo ya kujilinda wao na mali zao. Amelitaka jeshi hilo kukaa na uongozi wa wafanyabiashara hao kuona ni jinsi gani watamaliza kero zilizopo ikiwepo tishio la majambazi na usumbufu wa kwenye malori. Pia amewataka wafanyabiashara hao kutojaza mizigo na abiria kupita kiasi kwenye malori jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wafanyabiashara wa mnadani Mkoani Rukwa Ndugu E. Mazwile akizungumza katika kikao hicho ambapo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa kutenga muda wake na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Mkoa kwa kufika na kukutana na wafanyabiashara hao na kusikiliza kero zao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa (kushoto) akiwatambulisha viongozi mbalimbali walioambata na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kikao hicho.
Sehemu ya wafanyabiashara hao wa mnadani.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment