Nafasi Ya Matangazo

January 06, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na wananchi jijini Tanga (hawapo pichani) alipowasili katika Uwanja wa Tangamano, kwa ajili ya kukagua shughuli za wajasiriamali walionufaika na mikopo ya asilimia 10 pamoja na kuwakabidhi hundi za mikopo wajasiriamali hao.
Baadhi ya wananchi wa jiji la Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe (hayupo pichani) akizungumza na wananchi jijini Tanga, alipowasili katika Uwanja wa Tangamano kwa ajili ya kukagua shughuli za wajasiriamali walionufaika na mikopo ya asilimia 10 pamoja na kuwakabidhi hundi za mikopo wajasiriamali hao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali aliowakabidhi hundi ya mikopo ya asilimia 10, mara baada ya kukagua shughuli za wajasiriamali hao walionufaika na mikopo ya asilimia 10 mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe kuzungumza na wananchi (hawapo pichani) jijini Tanga katika Uwanja wa Tangamano.
Sehemu ya wananchi wakisikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian (hayupo pichani) wakati akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa Tangamano jijini Tanga.
***********
Na James Mwanamyoto - Tanga
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amekabidhi hundi yenye thamani ya Bilioni 2.761 kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vilivyonufaika na mkopo wa asilimia 10, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan aliyoitoa kwa wananchi kuwa ataitekeleza ndani ya siku 100 za uongozi wake.
 
Prof. Shemdoe amekabidhi hundi hiyo leo Januari 05, 2026 kwa vikundi hivyo jijini Tanga katika Uwanja wa Tangamano, mara baada ya kukagua shughuli za wajasiriamali walionufaika na mikopo ya asilimia 10 mkoani Tanga.
 
“Leo tumetoa Bilioni 2.761 kwa vikundi vya halmashauri ya jiji la Tanga, Korogwe Mji,  Korogwe wilaya , Lushoto, na Pangani, ambazo zitanufaisha vikundi vya wanawake 155, vijana 71 na wenye ulemavu 19 ambapo jumla ya ajira 1,715 zimetengenezwa,” amefafanua Prof. Shemdoe.
 
Prof. Shemdoe amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe, Balozi Dkt. Batilda Burian, kwa kusimamia vema utoaji wa mikopo ya asilimia 10 pamoja na kuandaa maonesho ya shughuli za vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo, na kuwaelekeza Wakuu wa Mikoa mingine kuandaa maonesho kama Mkoa wa Tanga ulivyofanya.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian amesema katika kutekeleza ahadi hiyo ya Mhe. Rais, kwa Tanga jiji pekee Prof. Shemdoe amekabidhi hundi ya Bilioni 2 kwa vikundi 137 ambapo wanufaika ni wananchi 686.
 
Naye mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo ya asilimia 10, Bi. Zainab Abdallah ambaye ni mlemavu amesema yeye na mwenzie Mariam Siafu wamenufaika na mikopo hiyo ambapo wameweza kununua bajaji nne (4), awamu ya kwanza walipata Shilingi Milioni 17 zilizowawesha kununua bajaji mbili (2) na awamu ya pili walipata Milioni 22 zilizowawezesha kununua bajaji (2) nyingine na hatimaye wamefanikiwa kuajiri madereva wanne (4).
Posted by MROKI On Tuesday, January 06, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo