Nafasi Ya Matangazo

July 09, 2014


Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishiriki  kubeba  nguzo
Vijana  wakishirikiana na mbunge  wao kubeba nguzo za umeme
jitihada za kupeleka  umeme  Lupingu  zikionekana
Mbunge wa jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe akiwa  chini ya shimo akiendelea  kuchimba shimo kwa ajili ya nguzo ya umeme kwenda  kata ya Lupingu kutoka Ludewa ,kushoto ni  diwani wa TLP kata ya Lupingu John Kiowi akishirikiana na mbunge huyo
Mbunge  Filikunjombe shimoni na diwani wa TLP  wakishiriki kuchimba mashimo ya nguzo za umeme
 
Mbunge  wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe akishiriki  kuchimba mashimo ya  nguzo za umeme pamoja na wananchi wa kata ya Lupingu
Na  Francis Godwin Blog
DIWANI  wa  chama   cha Tanzania Labour Party (TLP) kata ya  Lupingu  wilaya ya  Ludewa mkoani  Njombe  John Kiowi amempongeza  mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kwa jitihada zake   anazozifanya katika  kuwapelekea maendeleo wananchi wa Ludewa  huku akiwashangaa   wapinzani wanaopinga  jitihada  mbali mbali  zinazofanywa na serikali ya  chama  cha Mapinduzi (CCM) na  kudai  kuwa  yeye  si mpinzani wa uchwara wa  kupinga  maendeleo .

Akizungumza   na  wanahabari  jana wakati wa  zoezi la mbunge  Filikunjombe  na  diwani  huyo  kushiriki na  wananchi  wa kata ya  Lupingu  kuchimba mashimo ya nguzo  za umeme  na kusimika  nguzo hizo za umeme , Kiowi  alisema  kuwa   ni  zaidi ya  wabunge  watano  wamepata  kuliongoza  jimbo  hilo la Ludewa  ila ni mara  yake ya kwanza  kuona mbunge akishiriki bega kwa  bega na wananchi wake  kuchimba mashimo  kama ambavyo mbunge  huyo anafanya .

" Jamani  wananchi  kwanza ni jambo la kumpongeza mbunge  wetu mbali ya kuhimiza wananchi ila mwenyewe  pia amekuwa mstali wa mbele katika  kushiriki tofauti na wana siasa  wengine ambao  muda  wote  wao ni watu wa majukwaani ila  vitendo sifuri .....nasema  Ludewa  imempata mbunge na niweke  wazi  hapa mimi  sio mpinzani hivi  tujiulize wenyewe  nikisema mimi ni mpinzani napinga  nini hapa haya maendeleo  ni kwa  faida yangu na  wananchi  wote  sasa kama mbunge wa CCM wanafanya  kuna haja ya upinzani hapa "

Kiowi  alisema kuwa ataendelea  kufanya kazi na mbunge  Filikunjombe ikiwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata  yake kwani chama  chake  cha TLP katika  kata ya Lupingu  kinatekeleza  ilani ya  CCM ambacho  ndicho  chama  kilichopo madarakani na peke  yake  bila kumtegemea  mbunge hawezi  kufanya lolote.

Diwani Kiowi ambae  alikuwa amevalia  sare  za CCM katika  shughuli  hiyo ya maendeleo  alisema kuwa  katika kuhakikisha kuwa yeye  si mpinzani ila ni mpenda maendeleo  hata  sare za CCM zinazotolewa na mbunge Filikunjombe amekuwa akizivaa na amekuwa mstali wa  mbele kumpongeza  mbunge  huyo kutokana na kuwa mbunge wa mfano kwa kufanya kazi bila na makundi  yote .

Hata   hivyo  diwani  huyo alisema kuwa katika  suala la maendeleo hata  kuwa tayari kuona  watu  wachache  wakimkwamisha mbunge  huyo kwa  kushindwa kuunga mkono jitihada  zake katika kuwaletea maendeleo na kudai kuwa  kwa  upande  wake anaona  wapinzani ni  wana CCM wenyewe wasiopenda kujivunia maendeleo makubwa mbayo  mbunge  Filikunjombe ameyapeleka Ludewa .

Kwa  upande wake  mbunge  Filikunjombe mbali ya kumpongeza diwani  huyo wa TLP kwa  kushiriki  vema katika  shughuli za maendeleo bado  alisema kuwa ni  wapinzani wachache nchini ambao  wanajitoa kama  diwani  huyo katika  shughuli za maendeleo  zinazoitishwa na mbunge wa CCM

Alisema yapo  baadhi ya maeneo  wabunge ama madiwani wa upinzani  wamekuwa ni watu wa  kupinga kila jambo linalofanywa na mbunge ama diwani wa CCM  na  wengine  wasiokuwa na uzalendo  na Taifa  wamefikia hatua ya kubeza hata jitihada zinazofanywa na Rais Dr Jakaya  Kikwete katika  kuliletea maendeleo  Taifa  jambo ambalo si la kizalendo hata kidogo na kuwa  huo si upinzani wa kweli.

" Nataka  kusema  hivi wakati  wa kampeni ndio  wakati wa kupingana kisera ila baada ya chaguzi  hakuna  haja ya  kuendelea  kupingana ni kuwa  wamoja na kuwaletea  wananchi maendeleo hivi  hebu  niulize ujenzi huu wa barabara  ya Lupingu ,Ludewa  na Njombe Ludewa unaoendelea ni kwa  faida ya nani hii barabara  inatumiwa na wana CCM pekee  mbona  hata  wapinzani mnapita katika barabara  hiyo  hiyo  sasa unapinga  nini wakati  huu wa CCM kutekeleza ilani  yake ....tuwe  na uzalendo  wa nchi  yetu tusiwe wa  kupinga kila  kitu na mimi nikueleze  wazi kama  ungejaribu kupinga mradi huu wa umeme  kwa  kutoshiriki tungeonana  wabaya mbele ya  safari"

Akielezea  mradi huo wa umeme Filikunjombe  alisema kuwa kwa kasi  ambayo  wananchi  wanaenda nayo katika  kujitolea  nguvu  zao kuchimba mashimo na  kusogeza nguzo katika mashimo  hayo ni  wazi  mradi huo wa umeme  utakamilika kabla ya  Desemba mwaka  huu .

Aidha  alisema kuwa wakati akiingia madarakani mwaka 2010  ni  kijiji  kimoja pekee cha jimbo  hilo la Ludewa ambacho  kilikuwa na umeme  wa mafuta  ila  sasa  zaidi  ya vijiji 10  vina umeme na kuwa hadi sasa   jumla ya  vijiji 49 vitafikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa nguvu za  serikali ya Tanzania , Swedeni na kanisa na Romani Katoliki Dayosisi ya  Njombe.
Posted by MROKI On Wednesday, July 09, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo