Nafasi Ya Matangazo

July 09, 2014

 MKURUGENZI  Mkuu wa Taasisi ya Utafiti  wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), Dk. Mwele Malecela akiwa na Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka Wizara ya Afrya na Ustawi wa Jamii Upendo Mwingira pamoja na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Mpango wa END FUND ambao huchangisha fedha za kukabiliana na magonjwa hayo duniani wakiwa wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro walipokwenda kujionea juhudi za Serikali katika kukabiliana na magonjwa hayo.
 Baadhi ya watalii ambao ni wadau wa Mpango wa END FUND wakiangalia moja ya upasuaji wa jicho ikiwa ni juhudi za Serikali katika kukabiliana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele. Watali hao walipanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha.
Mratibu wa mpango wa Taifa wa Kukabiliana na Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Upendo Mwingira akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Olmolog Vet wilayani Siha mkoani Kilimanjaro walipokwenda kuwaangalia namna wanavyokabiliana na maambukizi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Posted by MROKI On Wednesday, July 09, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo