![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipTn7n1oRBKtSvBiot_cqBpoQPuQSKFBepSNX-VB80moXOrHEZi24UbqjESNyNQfSIys2H43vnq_whNzzabLp9WYbLjdUBFvtC1UFKnF8YvhJn0xV-eNpH5VLf3qRiSqGyLyANp1b6eYk/s1600/New+Picture+%282%29.png)
Mwandishi
na mtangazaji wa habari wa siku nyingi, Bwana Edward Kahurananga, amefariki
dunia hapo juzi tarehe 17/6/2014 baada
ya kuugua na kulazwa kwa muda mfupi.
Marehemu
Edward Kahurananga alizaliwa tarehe 25 Desemba, 1949 katika wilaya ya Kibondo
mkoani Kigoma. Alihitimu elimu ya Sekondari mwaka 1968 katika Sekondari ya
Livingstone iliyoko mkoani Kigoma.
Katika
uhai wake alisoma vyuo mbalimbali vya uandishi wa habari ndani na nje ya nchi.
Mwaka 1970 aliajiriwa na Radio Tanzania Dar es Salaam kama Mtangazaji Msaidizi
daraja la III. Alifanya kazi katika ngazi
mbalimbali katika mikoa katika mikoa kadhaa nchini chini ya Radio
Tanzania Dar es Salaam .
Baadaye
aliteuliwa kuwa Mhariri wa Habari Mkuu wa
Radio Tanzania Dar es Salaam kabla haijaunganishwa na Televisheni ya Taifa
kuunda TvT ambayo baadaye ilibadilishwa kuwa TBC. Mwaka 2004, Marehemu Edward Kahurananga alihamishiwa
Idara ya Habari-MAELEZO kama Afisa Habari Mkuu.Wakati ule Idara ya Habari
ilikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Tarehe
25 Desemba, 2009, Edward Kahurananga alistaafu kazi kwa mujibu wa kanuni za
Utumishi wa Umma wakati huo Idara ikiwa imehamishiwa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo.
Edward
Kahurananga alianza kuugua akiwa Mwanza na kulazwa katika hospitali ya Bugando
lakini akahamishiwa hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ambapo amefia tarehe 17
Juni, 2014 wakati wakiendelea kujaribu kuokoa maisha yake.Atazikwa kesho (Ijumaa)
tarehe 20 Juni, 2014 nyumbani kwake Vikindu jijini Dar es Salaam.
MUNGU
AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA
0 comments:
Post a Comment