Mzee Small afariki Dunia.
Habari za kusikitisha zilizotufikia hivi punde
zinaarifu kuwa Mwigizaji maarufu na mkongwe katika fani ya vichekesho nchini
Tanzania, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (59) amefariki dunia baada
ya kuugua kwa muda mrefu.
Mzee Small amefikwa na umauti majira ya saa 4 za
usiku wa Juni 7, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhumbili.
Akiongea kwa njia ya simu mke wa marehemu, Bi Fatuma
Saidi, ameithibitishia Father Kidevu Blog, kuwa Msanii Said Ngamba hatunae.
Bi Said amesema kuwa marehemu mumewe amefikwa na
umauti baada ya hali yake kubadilika jana (Juni 7) asubuhi na kumbikiza
Muhimbili ambako alishinda nae akipatiwa matibabu na majira ya saa tatu usiku
alirudi nyumbani na kumwacha kijana wake akimwangalia mgonjwa na ilipotimu saa
tano usiku kijano huyo alirudi na kusema baba amefariki.
“Nikweli Mzee Small amefariki”….yalikuwa ni
maneno machache yaliyobenba uchungu mzito kufuatia kifo cha mumewe.
Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.
Blog ya Father Kidevu inatoa pole kwa familia
yake yote, Ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.
MAISHA NA SANAA
Katika historia fupi, Mzee Small alipata elimu
ya msingi katika Shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa
mkongwe, Mzee Small kila ulipobahatika kuzungumza naye alikuwa na kawaida ya kutamba kuwa yeye ndiye msanii
wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.
Mzee Small alianza sanaa hiyo yapata miaka 31
iliyopita na alipata kufundishwa na mwigizaji Said Seif ‘Unono’ (ambaye pia kwa
sasa ni marehemu).
Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi
mbalimbali, Mzee Small wakati wa uhai wake ametumika katika vikundi vya
mashirika kama vile Reli, NASACO na mengine mengi, ambayo kwa sasa
hayajihusishi tena na shughuli hizo.
Mzee Small alianza kujulikana sana katika fani
ya uchekeshaji hasa pale alipoibuka na mchezo uliojulikana kama 50, 50, 100, na
ule wa Mjini Shule uliomwelezea mwanamke wa kijijini aliyeolewa mjini.
Mbali na kutamba na michezo hiyo, Mzee Small alikuwa
ni mcheshi na mwenye kupenda utani wakati wote, aliibuka na kichekesho
kisemacho Nani Mwenye Haki, ambacho baadaye alikiboresha zaidi.
Baadaye aliibuka na kitu kingine kikali
kilichokwenda kwa jina la Nani Kama Shule, huku akiwa amewashirikisha wakali
wengine kama King Majuto, Kingwendu na wachekeshaji wengine wanaotamba kwa sasa
Bongo.
Mzee Small alikuwa ndiye mmiliki wa kundi la
sanaa linalojulikana kama Afro-Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 kwenye
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kutoa ajira kwa vijana wa mitaani.
Pamoja na kuwa na uzoefu wa kisanaa, lakini
mkongwe huyo hakuwahi kuwa na mpango wa kujiunga na kundi lingine, ila alichokuwa
akifanya ni kurekodi na wasanii wengine alipokuwa akiitwa kwa makubaliano
maalum.
Pia mkali huyo wa vichekesho enzi za uzima wake
na uhai wake alikuwa akijishikiza katika duka moja Kariakoo la Home Shopping
Centre kimatangazo.
Kutokana na vichekesho, Mzee Small huwa anatania
kuwa sanaa ilimpa mke wa ndoa katika televisheni ambaye ni Bi Chau huku
akianisha kuwa mkewe, Bi Fatuma huwa hana tatizo lolote na Bi Chau kwani anajua
kinachoendelea kuwa ni kazi tu.
Mzee Small amefariki na kuacha mjane na watoto
watano, watatu wa kiume na wawili wa kike. Kipindi cha uhai wake Marehemu Small
alikuwa akisisitiza sana elimu na Sanaa iwe baada ya kumaliza masomo yao.
MATESO YA KIAFYA
Wakati akiendelea na harakati za kisanaa, mwaka juzi
Mzee Small aliripotiwa kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alipokuwa kwenye
shughuli za kisanaa Kanda Ziwa.
Ugonjwa huo ulimpa mateso makubwa huku akiwa
hana msaada wowote.
Wakati akiteseka na kiharusi alipata tatizo linguine
kwenye ubongo huku akitakiwa kila mwezi kwenda kliniki kwa ajili ya ‘check-.
Hakika kila nafsi itaonja mauti na leo Mzee
Small ambaye mbali na kuiburudisha alikuwa akitoa mafunzo kwa jamii yetu
kupitia kazi zake, leo ameonja mauti na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema
ampunzishe Mkali huyo wa vichekesho mahali pema.
REST IN PIECE MZEE SMALL, U WILL BE REMEMBERED FOREVER.
ReplyDelete