Meya wa Ilala, Jerry
Silaa akifungua rasmi tamasha la kuchangia damu katika viwanja vya
Stakishari, Majumbasita, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo ya siku 10
iliratibiwa na Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa (CCM).
Meya Silaa akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu
Salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wakiwemo wakina mama
wajawazito katika viwanja vya Sitakishari Majumbasita, Dar es Salaam.
Meya wa Ilala, Jerry Silaa akiugulia maumivu ya sindano
wakati akitoa damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali
mbalimbali wakiwemo wajawazito bila kuwasahau madereva na abiria wa bodaboda
wanaoandamwa na ajali.
Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa naye akidhihirisha azma
yake ya kuchangia damu kwa vitendo katika kilele cha kampeni yake ya kuchangia
damu jana katika viwanja vya Sitakishari, Majumbasita ambapo mamia ya wakazi wa
Dar es Salaam walijitokeza.
Mwakilishi wa Chuo cha Diplomasia, Kennedy Ndosi
(katikati) aliyewahamasisha wanafunzi wa
Chuo hicho waliofika kuchangia damu akiwasikiliza Meya Silaa na Diwani Bonnah
wakati wa tamasha hilo.Meya Silaa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dk Willy
Sangu (kulia) wakiondoka baada ya kumaliza zoezi la kuchangia damu katika
tamasha lililoandaliwa na Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa katika Viwanja vya
Sitakishari leo.




0 comments:
Post a Comment