Nafasi Ya Matangazo

June 12, 2014

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Push Media Mobile Limited imeanzisha kitengo maalum cha kuhudumia taasisi za Kijamii kupata taarifa mbalimbali kijulikanacho kwa jina la Push for Change. Kwa kupitia huduma hiyo, taaasisi za kijamii sasa zinaweza kupata taarifa mbali mbali kwa kupitia njia za mawasiliano na pamoja na simu za mkononi. Ili kujiunga na huduma hiyo, unatakiwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kucha gua huduma unayotaka. Mbali ya kupata taarifa na huduma, kwa kupitia programu ya Push For Change, taasisi za kijamii pia zinaweza kuunganishwa na washiriki wengine wa hapa hapa nchini na nje ya nchi kwa njia mbali mbali za mawasiliano pamoja na simu za mkononi. Akizungumza katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na taasisi zaidi ya 62 zikiwemo za umoja wa mataifa,  Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile Limited, Freddie Manento alisema kuwa lengo la kuanzisha huduma hiyo ni kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbali mbali kwa taasisi za kijamii (non-profit organization) na kuyaunganisha na taasisi nyingine za aina hiyo duniani kupitia teknolojia ya kisasa. Manento alisema kuwa sekta ya mawasiliano duniani imekuwa na inaendelea kupanuka na kuwafanya wao kubuni njia mbalimbali ambazo zintaweza kuunganisha jamii katika kupata taarifa kama za uchumi, biashara, afya, michezo na burudani, savei, elimu na kilimo, utaliii na nyinginezo. “Mtandao wa simu ya mkononi umefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini na bara la Afrika, umerahisisha sana upatikanaji wa taarifa, tena kwa bei nafuu, takwimu zinaonyesha kuwa mpaka sasa kuna watumiaji simu za mkononi milioni 761 ambao wanaweza kupata taarifa katika mazingira mazuri na hata wanaoishi katika mazingira magumu, hivyo progamu hii itawafikia watu wengi zaidi na kwa haraka zaidi,” alisema Manento. “Tumetumia teknolojia ya kisasa katika kufanikisha huduma hii kuiwezesha jamii kwa haraka zaidi kutokana na ushirikiano na wadau wetu mbali mbali katika huduma ya kijamii nchini na nje ya mipaka ya nchi, taarifa hizi zinaweza kupatikana kwa njia ya redio na televisheni mbali ya njia nyingine za mawasiliano,” aliongeza.
Posted by MROKI On Thursday, June 12, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo