Mkurugenzi mtendaji wa AzamTV, Rhys Torrington alisema:
Lengo kuu la kufanya shindano hili ni kuamsha hisia za mashabiki wa soka na
kuonyesha umuhimu wa kuthamini mashabiki kwa sababu bila wao mpira wa miguu
usingekuwepo leo hii
Mratibu wa Shindano hilo Wasiwasi Mwabuklambo akizungumza
AzamTV
leo wamezindua mashindano yatakayowahusisha wapenzi wa kandanda
yatakayojulikana kama KWETU HOUSE. Mashindano haya ambayo ni mara
ya kwanza Tanzania yatashirikisha wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu
ambapo watu kumi wa 10 wa timu mbalimbali watachaguliwa na kuishi katika
nyumba moja kwa muda wa siku 3 wakionyesha ni jinsi gani wao ni mashabiki namba
mmoja kwa timu zao .
Akizindua
mashindano hayo, Mkurugenzi mtendaji wa AzamTV, bwana Rhys Torrington alisema:
Lengo kuu la kufanya shindano hili ni kuamsha hisia za mashabiki wa soka na
kuonyesha umuhimu wa kuthamini mashabiki kwa sababu bila wao mpira wa miguu
usingekuwepo leo hii; wakati huo huo ni kuwaletea watazamaji vipindi
vinavyoburudisha na kuelimisha.
Mashindano
haya yametokana na ubunifu wa wafanyakazi wa Azamtv ambapo hiki ni kipindi
kimojawapo kitakachofuatiwa na vingine vingi ambavyo viko ndani ya maandalizi
kupitia kampuni ya Uhai Production ambayo ni kampuni mama ya AzamTV; aliongeza
bwana Wasiwasi Mwabulambo ambaye ni mratibu wa mashindano hayo.
Wanaoruhusiwa
kushiriki mashindano haya ni wanaume wenye umri wa miaka kumi na nane (18) na
kuendelea.
Wakiwa
ndani ya jumba la KWETU HOUSE washiriki wataenguliwa kila siku ya jumapili
mpaka kubakia washiriki watatu ambapo mmoja wao atajinyakulia kitita cha
shilingi milioni kumi (10)
Usaili
wa shindano hili utafanyika siku ya jumamosi tarehe 24/05/2014 uwanja
wa Leaders club, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Usaili utakuwa
ni bure.
Pia
mashabiki wanaweza kujisajili kwa kutuma video zao fupi kwenda kwenye whatsApp
number 0759 38 65 68 nakuonyesha ushabiki wao wa dhati.
Watakaochaguliwa
watatangazwa tarehe 27/05/2014 ambapo wataingia ndani ya jumba la KWETU HOUSE
tarehe 30/05/2014; na mshindi atapatikana tarehe 27/06/2014.
Shindano
hili limedhaminiwa na Azam Energy Drink kwa ushirikiano wa Channel Ten, Magic
Fm na Times Fm.
0 comments:
Post a Comment