Baloziwa Tanzania
chini Nigeria Mh. Daniel Ole Njoolay akifungua kongamano la Biashara na uwekezaji
katika Hoteli ya Sheraton jijini Abuja Nigeria ikiwa nisehemu yasherehe za maadhimisho
ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizoandaliwa na ofisi ya ubalozi
wa Tanzania nchini Nigeria.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
wa TTB, Teddy Mapunda akizungumza wakati Alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu vivutio
vya utalii vya Tanzania katika kongamano la biashara na uwekezaji jijini
Abija Nigeria juzi.(Na Mpigapicha wetu
Mh. Daniel Ole
Njoolay, Baloziwa Tanzania nchini Nigeria akikata keki huku akishuhudiwa na mwakilishi
wa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (wapilikulia)
na baadhi mabalozi wanao wakilisha nchi zao Nigeria katika tafrija iliyotayarishwa
na ubalozi wa Tanzania kusherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar zilizofanyika katika
hotel ya Sheraton jijini Abuja Nigeria.
*********
Na Geofrey Tengeneza – Abuja Nigeria
Jumuiya ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi
wa Nigeria kwa ujumla, wameombwa kuja kuwekeza kwa ujumla na kutembelea vivutio
vya utalii mbalima livinavyopatikana nchini Tanzania.
Hayo ya mesemwa na Balozi wa Tanzania nchini
Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay katika maadhimisho ya miaka hamsini 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) yalioandaliwa na ofisi ya ubalozi
wa Tanzania nchini Nigeria nakufanyika katika Hoteliya Sheraton jijini Abuja.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo la
Biashara naUwekezaji, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole
Njoolay amesema Tanzania inajivunia muungano wake ulioasisiwa na Hayati Baba wa
Taifa la Tanzania Mwl Julius Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa
Zanzibar mnamo tarehe 26 April, 1964 ambao sasa umetimia miaka 50.
“Watanzania tuna jivunia sana muungano wetu kwani
niwakipekee sana hapa barani Afrika, nani muungano uliodumu kwa muda mrefu zaidi
kuliko muungano wowote ule Barani Afrika” alisema Balozi Njoolay.
Akizungumzia kuhusu fursa za biashara Mkurugenzi
wa maendeleo ya biashara wa TANTRADE Bwana Edwin Rutageruka amesema kwamba mahusiano
ya kibiashara kati ya nchi hizimbili yameendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kwamba
Tanzania imedhamiria kuendelea kukuza biashara katiyake na Nigeria.
Naye Mkurugenzi wamipango na maendeleo wa mamlakaya
EPZ Bwana Lamau Mpolo ameelezea uwepowa fursanyingi za uwekezaji katika sektambalimbali ikiwemo ya gesi na madini. Ameelezea pia namna serikaliya Tanzania
ilivyoweka mazingira mazuri kwaajili ya kuvutia wawekezaji kutoka duniani kote katika sekta mbalimbali za uchumi nchini
Tanzania.
Akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii vya
Tanzania vilivyomo katika orodha ya maajabu ya 7 yaasili barani Africa,
Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Bibi Teddy Mapunda amesema pamoja na vivutio
vitatu (3) vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Crater ya Ngorongoro na Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti, Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi zaidi na vya kipekee
na akabainisha kuwa imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutangaza vivutio vyake
saba vya asili ambavyo pamoja na vile vilivyomo katika maajabu Saba ya asili barani
Afrika, vivutio vingine nihifadhi ya taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Kituro,
hifadhi ya Taifa ya Gombena Pori la akiba la Selous.
Amewakaribisha wananchi wa Nigeria kutembelea
Tanzania na kujionea uzuri na upekee wavivutio vya Tanzania sambamba na kuwekeza
katikasekta ya utalii.
Kongamano hilo lililohudhuriwa na takribani wawekezaji
na wafanyabiashara kutoka Nigeria mia moja lilifuatiwa na tafrija iliyofanyika usiku
katika hoteli hiyo n akuhudhuriwa na waalikwa takribani 350 wakiwemo Mabalozi wa
mataifambalimbali nchi Nigeria, wagenikadhaa mashuhuri na baadhi ya watanzania waishio
nchini Nigeria.
0 comments:
Post a Comment