Nafasi Ya Matangazo

April 06, 2014

Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kushoto) akikabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) na Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kushoto) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakati wa kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.


Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dkt.  Hemid Nassoro akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mahumbika kabla ya kupokea msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.
Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila hivi karibuni.

 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakifurahia jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.



Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.



Wasanii wa kikundi cha ngoma na maigizo cha kijiji cha Mahumbika, Lindi wakitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.



Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (wa nne kulia waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dkt.  Hemid Nassoro (kushoto kwa mkuu wa mkoa), Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kulia kwa mkuu wa mkoa) pamoja na viongozi na walimu wa Wilaya ya Lindi wakati wa kukabididhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.



Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (wa pili kulia) na Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (wa pili kushoto) wakipongezwa na wazee wa kijiji cha Mahumbika mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.
Posted by MROKI On Sunday, April 06, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo