Nafasi Ya Matangazo

April 06, 2014

 Wachezaji wa Tanzania wakishangilia ushindi wao na kutinga Fainali za michuano ya dunia kwa watoto wanaoishi mazingira magumu.
Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania (pichani juu)  imetinga fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya kuichapa Marekani mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Hadi mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao 4-0. Bao pekee la Marekani katika mchezo huo ambayo hadi nusu fainali ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za mwisho.

Kwa matokeo hayo, Tanzania inacheza nusu fainali na Burundi. Mechi hiyo inachezwa leo (Aprili 6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika nusu fainali ya pili.

Mchezo huo wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi  akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.

Katika mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo, Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2.
Posted by MROKI On Sunday, April 06, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo