Nafasi Ya Matangazo

April 28, 2014

Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani akihojiwa na waandishi wa habari katika hafla ya kuhamsidha jamii kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa sikoseli 'seli mundu' iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ugonjwa  wa sikoseli hurithiwa kutoka kwa wazazi wote wawili wenye vinasaba vya ugonjwa huo.
 Mmoja wa wagonjwa wa sikoseli, Arafa Said Salim ambaye pia ni muasisi wa Jumuiya ya wagonjwa wa Sikoseli Tanzania (CDPCT) akizungumza kuhusu ni jinsi gani mtu anayeugua ugonjwa huo anaweza kuishi maisha ya kawaida. Inaelezwa watoto kati ya 8,000 na 11,000 huzaliwa na ugonjwa huo kila mwaka nchini.
 Mmoja wa wagonjwa wa sikoseli, Arafa Said Salim akipozi kwa picha na mumewe, Salim Msaky ambaye yeye hana sikoseli hafla hiyo. Hiyo ni kuonyesha kuwa mgonjwa wa sikoseli anaweza kuolewa ama kuoa mwenza asiye na ugonjwa huo bila kuleta madhara kwake.
Mkurugenzi wa Kituo cha Little Fingers Music, Veronica  Eyakuze akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Posted by MROKI On Monday, April 28, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo