Nafasi Ya Matangazo

April 04, 2014

Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani akiongea jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA). Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina, pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba.
Kamishana wa zamani wa Tume ya Uchaguzi  ya Zanzibar - ZEC, Dkt. Nassor Seif Amour akitoa ufafanuzi  jijini Dar es Salaam jana Aprili 3, 2014 katika wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).  Pembeni ni Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba akitoa maelezo jinsi vyombo vya habari vinavyoshiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya, wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Washiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Rioba akitoa maelezo jinsi vyombo vya habari vinavyoshiriki katika mchakato wa kupata katiba mpya, wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Washiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Washiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHWashiriki walioshiriki katika mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya The  Open Society Initiative  For  Eastern African Tanzania  (OSIEA).
Wadau wakitoa michango yao katika mjadala huo.
Wadau wakitoa michango yao katika mjadala huo.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa akiuliza swali mara baada ya majadiliano.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dr Wilbroad Slaa akijadili jambo na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba (kushoto) na Mwenyekiti wa Mjadala huo, Profesa Chris Maina (kati).

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Mstaafu Augustino Ramadhani amewataka wajumbe wa bunge maalumu la katiba kujadili vipengele vya rasimu hiyo kwa kuviboresha badala ya kulumbana.
Jaji Ramadhani ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mjadala kuhusiana na umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya kipekee, Mjadala ulioandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya OSIEA.
Amesema kuwa, tume ya mabadiliko ya katiba imefanyakazi yake ya kuwasikiliza wananchi na kuandika rasimu ambayo ipo mbele ya wajumbe hao, na hivyo kutoa wito kwao kujadili kwa makuni ili kutengeneza mustakabali mzuri wa Tanzania kwa kuzingatia hoja na kila upande wa Muungano. 
“Sisi kama tume tumefanya kwa kadiri ya uwezo wetu na tumepata rasimu ya pili, sasa ni jukumu la wajumbe wa bunge la katiba kujadili na kuboresha vipengele vilivyomo kwenye rasimu hiyo na kuachana na malumbano”. Alisema Jaji Ramadhani.
“kila mmoja akitaka kipengele chake kiwemo kwenye rasimu hiyo, ni jambo lisilowezekana, kinachotakiwa hapa ni wajumbe kujadili na kupendekeza mambo yenye maslahi kwa taifa kwa sasa na baadae”. Alisisitiza Jaji Ramadhani
Jaji Ramadhni amesema, vipengele vinavyobishaniwa vinajadilika na vinaweza kuboreshwa zaidi kwa malahi ya pande zote mbili ili kupata katiba yenye kutoa nafasi kwa kila upande wa Muungano katika kushiriki katika ujenzi wa taifa.
“Vipengele vinavyoshindaniwa vinafaamika na wajumbe wanaweza kutumia busara kuvijadili na kuvitolea maamuzi kwa manufaa ya nchi ambayo inasubiri kwa hamu Katiba Mpya” alisema Jaji Ramadhani.
Akiongelea nafasi ya vyombo vya habari kwenye mchakto huo Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr Ayoub Rioba amesema, bado vyombo vya habari havijapewa nafasi ya kutosha kisheria kushiriki katika kuelimisha umma kuhusiana na mchakato huo.
“ Vyombo vya habari bado havijapewa nafasi yoyote kwenye mchakato huu bali vinafanya kazi kwa mazoea na pia kuna vipingamizi vingi vinawekwa kuwazuia waandishi wa habri kuandika habari za bunge la katiba” alisema Dr Rioba.
Kamishana wa zamani wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar –ZEC, Dr Nassor Seif Amour amwataka wajumbe wa Bunge la katiba kuzingatia matakwa ya wananchi badala ya kujadili maoni yao binafsi ama matakwa ya vyama wanavyoviwakilisha.
“Sisi tunawakumbusha wajumbe wa bunge maalumu la katiba kukumbuka maoni wanayoyajidili kuwa ni ya wananchi sasa wasiweke maoni yao ama ya chama katika mchakato huu ili wasitunge rasimu mpya badala ya kuiboresha”. Alisema Dr. Nassor.
Mjadala huo umehudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya wananchi, asasi za kiraia na wanasiasa.
Posted by MROKI On Friday, April 04, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo