Baadhi ya wajumbe wa TASWA wakipiga kura kuwachagua viongozi mbalimbali wa kukiongoza chama hicho. Mroki Mroki, Mwani Nyangasa na Amiri Mhando ni miongoni mwa wateule wapya.
Safu mpya ya Viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) waliochaguliwa hii leo.
********
JUMA
Abbas Pinto amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) baada ya mpinzani
wake George John Ishabairu kujitoa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo
kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
George alitangaza kujitoa baada ya kufika ukumbini, akisema kwamba Mwajiri wake, Wizara ya Maji amemwambia ajitoe.
Pinto
alipata kura 82 wakati 13 zilimkataa, na Egbert Mkoko ameshinda nafasi
ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 67 dhidi ya 32 za Mohammed Omary Masenga.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Wambura Mgoyo alimtaja Amir Mhando kushinda tena nafasi ya Ukatibu Mkuu baada ya kupata kura 93. Mhando hakuwa na mpinzani na kura mbili tu zilimkataa.
Nafasi ya Katibu Msaidizi imekwenda kwa Grace Aloyce Hoka aliyepata kura 65 dhidi ya 31 za Alfred Lucas Mapunda.
Mweka
Hazina Msaidizi Zena Suleiman Chande amepata kura 55 dhidi ya 40 za
Elius John Kambili, Mweka Hazina Shija Richard Shija amepata kura 57
dhidi ya 38 za Mohamed Salim Mkangara.
Walioshinda nafasi za Ujumbe ni Ibrahim Mkomwa Bakari, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa na Urick Chacha Maginga.
0 comments:
Post a Comment