Nafasi Ya Matangazo

March 08, 2014

Kumekuwa na muendelezo wa matukio kadhaa kutoka kwa kikundi cha watu kumuhusisha Mh Lowassa na matukio ya uongo na kumzushia vitu vya ajabu  kabisa, hususani katika mitandao ya kijamii.
 
Kumesambazwa picha ya noti ya shilingi Mia tano yenye picha ya Mh Lowassa.Kitendo hicho siyo Utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama za   utaifa na mamlaka ya nchi.
 
Mh Lowassa anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya mitandao ya kijamii,   lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi kutumia nguvu hiyo ya mitandao   kwa kujadili maendeleo ya nchi yetu badala ya kuwa watu wa kuzusha mambo  yasiyo na tija kwa nchi yetu.

  Imetolewa na ofisi ya Mh lowassa(mb)
Posted by MROKI On Saturday, March 08, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo