Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ridhwan Kikwete
akionesha fomu aliyochukua ya kugombea ubunge jimbo la hilo kulia kwake ni
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo, Kongo Kamate na Mbunge wa viti maalum wa
jimbo la Charinze Subira Mgalu.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akijaza fomu
ya kugombea jimbo hilo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete akiongozana na wanachama wa CCM kwenda kuchukua fomu fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya Bagamoyo.
* ********** *
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhwan Kikwete jana alichukua fomu katika
ofisi za msimamizi wa uchaguzi wilayani
Bagamoyo na leo anatarajia kurudisha fomu hiyo.
Akisindikizwa na mamia ya wanachama na
mashabiki wa CCM wa jimbo la Chalinze na Bagamoyo, Ridhwani alimhakikishia ofisa wa uchaguzi wa wilaya ya Bagamoyo Shija
Andrew, kuwa atazingatia taratibu zote za uchaguzi na kutoendesha kampeni za
matusi na vurugu.
Baada ya kuchukua fomu hiyo pamoja na
nakala nyingine muhimu za uchaguzi aliongozana tena na mamia ya wafuasi wake
kuelekea kwenye ofisi za CCM Bagamoyo ambapo alizungumza na waandishi wa
habari.
Katika mazungumzo yake hayo Ridhwan alitaja
vipaumbele vyake kwa kuleta maendeleo kwa wakazi wa Chalinze ambapo
alisisitizia kuimarisha upatikanaji wa maji salama na ya uhakika, kuimarisha
afya, elimu pamoja na kukuza ajira kwa vijana.
"Kama
mnavyofahamu kuwa Chalinze ni eneo ambalo linakabiliwa na changamoto
nyingi kama vile maji, umeme na hata suala zima la ajira kwa vijana sasa pindi
ambapo nikipata Ubunge kwangu mimi nitahakikisha kuwa napunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo hilo"alisema
Ridhwan.
Aliongeza kuwa "Mimi nimeguswa na changamoto mbalimbali zinazowakuta wakazi wa wilaya hii na kama ambavyo nilisema kuwa sikushinikizwa ila ni kwa matakwa yangu mwenyewe naona kabisa kuwa nipo katika hali na nguvu ya kushirikiana na wananchi kumaliza shida za Chalinze".
Aliongeza kuwa "Mimi nimeguswa na changamoto mbalimbali zinazowakuta wakazi wa wilaya hii na kama ambavyo nilisema kuwa sikushinikizwa ila ni kwa matakwa yangu mwenyewe naona kabisa kuwa nipo katika hali na nguvu ya kushirikiana na wananchi kumaliza shida za Chalinze".
Ridhwan pia alisema kuwa atasaidia kutatua
ugomvi wa mara kwa mara unaowakumba wakulima na wafugaji na kuwataka wakazi wa
Chalinze kumchagua kwa kishindo. Wakati huo huo mgombea wa Ubunge wa jimbo
hilo kwa tiketi ya Chadema Matayo Torongey akizungumza baada ya kuchukua fomu
alisema kuwa anavyo vipaumbele vingi kimojawapo ikiwa ni kuinua maisha ya
wakazi wa Chalinze.
Leo Ridhwan anatarajiwa kurejesha fomu za
kugombea ubunge katika ofisi ndogo za uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment