Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali leo amefungua rasmi Tamasha la kwanza la Mwanamke na Akiba jijini Dar es Salaam leo. Tamssha hilo linalofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala litaambatana na mafunzo ya aina mbalimbali za ujasiriamali na uwekaji akiba kwa manufaa ya baade.
Mkurugenzi Mtentandaji wa Angels Moment, Naima Malima akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo.
Wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wakifuatilia hotuba za ufunguzi wa Tamasha la Mwanamke na Akiba.
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda (kulia) akiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, Regina Lowasa wakifuatilia uzinfduzi huo wa tamasha la Mwanamke na Akiba.
Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali akionesha tuzo aliyiopewa na Mkurugenzi Mtentandaji wa Angels Moment, Naima Malima.
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda akiangalia Tuzo aliyopewa mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali.
Mke wa Makamu wa Rais akimkabidhi tuzo kiongozi wa Umoja wa wake wa viongozi, Germina Lukuvi.
Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali, akimkabidhi cheti cha shukrani ofisa wa Azam
Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali, akimkabidhi cheti cha shukrani Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele.
Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali akimkabidhi cheti Afisa wa PSPF, Delphin Richard.
Picha ya pamoja ya wazamini na waandaaji pamoja na mgeni rasmi.
Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali akikata utepe kuzindua Tamasha la Mwanamke na Akiba. Kushoto ni Mwaandaaji wa Tamasha hilo na Mkurugenzi Mtentandaji wa Angels Moment, Naima Malima.
Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali (kulia) akisikiliza
maelezo ya namna asali inavyozaklishwa hadi kuingizwa sokoni kutoka kwa Mke wa
Waziri Mkuu, Tunu Pinda jana wakati akitembelea mabanda ya maonyesho katika tamasha
la Mwanamke na akiba lililoanza Mbagala jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni
wake wa viongozi .
Mama Asha Bilali akipiga picha na wafanyakazi wa PSPF ambao nao wapo hapo kuhamasisha wakina mama hao kujiunga na Fao la hiari la Mfuko wa Pensheni wa PSPF ambapo kujiunga ni kuanzia sh 10,000/= tu.
PPF nao wapo katika maonesho hayo na hapa nao wakilamba picha na mgeni rasmi.
0 comments:
Post a Comment