Mkurugenzi
wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon
Mollel akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga msaada wa
Tani nne za unga wenye thamani ya shilingi Milioni 4.2,baada ya wilaya
yake kupata maafa yaliyotokana na mvu zilizoambatana na upepo mkali na
kusababisha badhii ya watu kukosa nyumba za kuishi
Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga Arusha Philemon Mollel akiongea mbele ya wanakijiji(hawapo pichani)namna
alivyoguswa na maafa hayo yaliyopelekea kutoa msaada huo huku kiwataka
wafanyabishara,makampuni,watu binafsi kujitokeza kuwasaidia waanga wa
maafa hao,mbali na msaada huo wa tani nne za unga pia alitoa shilingi Milioni moja kwaajili ya waanga
Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akiwa na ugeni
mzito kutoka kampuni ya Monaban ofisini kwake,lengo la ugeni huo nikutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa maafa ya mvua
Mkurugenzi
wa Monaban kushoto Philemon Mollel akiongelea namna alivyoguswa na
maafa hayo ambayo yalisababisha baadhi ya watu kukosa makazi ,
Kina mama ambao ndio waathirika wa kubwa wa maafa hayo wakisubiria zoezi la kugawiwa chakula cha msaada
Mtendaji wa kijiji Bi.Trea Ramadhani akitoa shukrani zake za dhati kwa mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichipo Arusha
Afisa
Tarafa Masama Bw.Nsajigwa Ndagile akisoma taarifa ya madhara
yaliyotokana na mvua hiyo kuwa ni pamoja na kuezuliwa kwa mapaa ya
nyumba,kubomolewa kwa kuta za nyumba na kuharibiwa kwa mazao hasa
migomba hali iliyosababisha baadhi ya kaya kukosa mahali pa kulala hivyo
kujihifadhi kwa majirani
Wanakijiji wakishuhudia msaada ulioletwa kijijini kwao
Mkuu
wa wilaya Novatus Makunga
akimkabidhi msaada uliotolewa na kampuni ya Monaban ,mtendaji wa kijiji
cha kwa sadala Bi.Trea Ramadhani msaada uliogharimu zaidi ya milioni 4,Kushoto ni kaimu mkurugenzi Bw.Zabdieli Moshi
Mkuu
wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akitoa shukrani zake za dhati kwa
mmiliki wa kiwanda cha Monaban kwa kuweza kuwaletea chakula cha msaada
na kuwataka makampuni,mashirika na watu binafsi kuiga mfano wa Monaban
kwa kuwasaidia waanga wa maafa yaliyotokana na mvua zilizoambatana na
upepo mkali na kusababisha watu kukosa makazi hivi karibuni ktika wilaya yake
Mama
ambaye ni muathirika wa maafa hayo akitoa shukurani zake kwa mkurugenzi
wa kampuni ya Monaban kwa kuweza kuwakumbuka kipindi cha shida na kudai
kuwa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli
Nyumba ya familia ya Bibi Aziza Mohammed baada ya kuezuliwa paa
Bibi
Aziza Mohammed kama anavyooneka katika picha baada ya mvua kusababisha
mafaa makubwa kwake hali iliyosababisha yeye kuishi chooni na mjuuku wake
Wanakijiji wakiwa wanashusha mifuko ya unga ndani ya gari
(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
0 comments:
Post a Comment