Nguku anaelezea kwamba kitabu hicho yenye kauli mbiu “Sio
Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi,” inatoa hamasa kwa watu hasa hasa kundi la vijana waweze kuwa na uthubutu wa kutimiza malengo
yao katika maisha. Wanaoshuhudia ni mama yake mkubwa Bi. Anna Kikwa na baba yake mdogo Bw. Emmanuel Mallewo.
************
Vijana
wakitanzania wameaswa kuacha kulalamika na kuishi katika maisha ya nadharia,
badala yake wameshauriwa kubadilika kuwa watendaji na wenye uthubutu wa kutimiza
malengo yao katika maisha.
Maneno hayo yalisemwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa Amajat Investment Bw. Aman Nguku jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa kitabu chake kiitwacho ‘Safari Ya Ndoto’ inayobeba kauli mbiu “Sio Serikali ni Mimi, Wewe na Sisi.”
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Nguku alisema imefika wakati sasa
watanzania hasahasa kundi la vijana waamke kutoka usingizini na kutimiza
malengo yao ya kimaisha ambayo wanapenda kufikia.
“Imetosha kusema kesho,
kufikiri bila kutenda na kuongea bila vitendo. Kinachotakiwa ni kuanza
utekelezaji,” alinukuu Bw. Nguku kutoka kwenye kitabu chake chenye kurasa 108.
Akielezea madhumuni ya
kuandika kitabu hicho, Bw. Nguku ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu
anayesomea shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam
alisema:
“Hiki kitabu ni
mahususi kwa wale watu ambao wana ndoto mbali mbali katika maisha yao lakini
hawajui pakuanzia, iwe ndoto ya kuwa mfanyabiashara maarufu, mwanasiasa au
daktari bingwa. Hiki kitabu ni ramani maalum kwao.”
Aliendelea, “Kitabu
hiki kinaweza pia kuwa changamoto kwa wale ambao wamekata tamaa katika maisha.
Kwa kusoma maandishi ya kitabu hiki, wanaweza wakafufua ndoto zao na kufanikiwa
katika yale waliyoyapanga.”
‘Safari
Ya Ndoto’ pia inabeba dondoo kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere, mfanyabiashara maarufu Bw. Reginald Mengi na Mkurugenzi
Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Bw. Patrick Ngowi.
Kitabu hiki
kinasambazwa katika maduka mbali mbali jijini Dar es Salaam na nchi nzima ili
watanzania wengi wapate kukisoma. Kinauzwa kwa Tsh 5000 tu.
Kwa sasa, mtunzi Nguku
pia anaandika vitabu vingine viwili venye vichwa ‘Ndogo lakini muhimu, kesho’ na ‘What is life for!’ (Maisha ni
ya nini!).
0 comments:
Post a Comment