Kufuatia tukio la maafa lilotokea Kilosa Morogoro,
kampuni ya bima ya AAR yaungana na serikali kusaidia wahanga wa
mafuriko walipoteza makazi yao na wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Kampuni iyo ilichangia vyakula mbalimbali kama vile mchele, maharage na mafuta ya kupikia yenye thamani ya shilingi milioni 3 za kitanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari Afisa Uhusiano wa AAR , Amisa Juma alisema " Tumekuja hapa leo kwa sababu tumeguswa na kilichotokea kwa waathirika wa mafuriko,na tumeona umuhimu wa kuwatembelea na kutoa rambirambi kwa wahanaga hawa.
Wafanyakazi wa AAR walipata mapokezi mazuri kutoka kwa Mkuu wa Wilaya w Kilosa Mhe. Elias Tarimo ambaye alitoa taarifa fupi kuhusiana na mafuriko hayo pia alitoa shukurani zake za dhati kwa kampuni kwa kutoa msaada huo wa chakula.
“Tungependa kutoa shukrani zetu za dhati kwa AAR insurance kwa kushirikiana nasi katika janga hili pia ngependa kutoa wito kwa makapuni ya kiserikali na yasio ya kiserikali kutoa misaada zaidi kwa wahanaga hawa wa mafuriko ,kwa sasa wanamahitaji ya makazi , kwa vile wengi wao waliopotea makazi yao . Ni wajibu wetu kuisaidia jamii katika njia yeyote tunayoweza kwa kua hili ni janaga la taifa, alisema Mhe.Elias Tarimo , Mkuu wa Wilaya ya Kilosa .
0 comments:
Post a Comment