Deni la Taifa linasimamiwa kwa kuzingatia Sheria
ya Mikopo, Dhamana na Misaada ya mwaka 1974 kama ilivyorekebishwa mwaka 2003 na
Mkakati wa Madeni wa mwaka 2002.
Aidha, deni la Taifa linajumuisha deni la
Serikali la ndani na la nje pamoja na deni la nje kwa Sekta binafsi.
Hadi kufikia Desemba, 2013, Deni la Taifa
limefikia Dola za Marekani bilioni 17.10 sawa na shilingi trilioni 27.04 Kati
ya kiasi hicho, Deni la Nje ni Dola za Marekani bilioni 12.79 sawa na shilingi
trilioni 20.23 ambazo ni asilimia 74.81 ya Deni la Taifa. Aidha Deni la ndani
ni shilingi trilioni 6.81 ambazo ni sawa na asilimia 25.19 ya Deni la Taifa .
Kati ya Deni la Nje la Taifa, Dola za marekani bilioni 10.563 sawa na shilingi
trilioni 16.71 ni deni la Serikali na Dola za Marekani bilioni 2.23 sawa na
shilingi trilioni 3.52 ni Deni la Sekta Binafsi. SOMA ZAIDI HAZINA
0 comments:
Post a Comment